Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yasaidia jeshi la Sudan Kusini kutathmini kesi dhidi ya askari

Machafuko yamesababisha watu kukimbia maeneo ya vijijini karibu na Yei jimbo la Equatoria kati, Sudan Kusini.
UNMISS/Nektarios Markogiannis
Machafuko yamesababisha watu kukimbia maeneo ya vijijini karibu na Yei jimbo la Equatoria kati, Sudan Kusini.

UNMISS yasaidia jeshi la Sudan Kusini kutathmini kesi dhidi ya askari

Sheria na Kuzuia Uhalifu

Timu kutoka Kurugenzi ya Haki Sheria ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF) mwishoni mwa wiki kwa usaidizi wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), imehitimisha tathmini yake katika Kaunti ya Maridi jimboni Equatorial Magharibi kutathmini kesi zinazohusisha wanajeshi wa nchi hiyo.

Tathimini itawezesha kufunguliwa mashtaka kwa askari wa jeshi ambao wanashukiwa kufanya uhalifu mkubwa, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kingono na aina nyingine za unyanyasaji wa kijinsia.

Mama Sarah Bennert, mwanaharakati na mwakilishi wa wanawake anasema hatua hii inawakilisha ishara ya haki na uwajibikaji, "tuna masuala mengi yanayotukabili hapa kama wanawake. Wakati mwingine unaripoti kesi na haki imechelewa na unabaki kukata tamaa na bila msaada wowote. Sasa, kwa uwepo wa timu ya tathmini hapa chini tunatumai kesi hizo zote walizozizingatia zitasikilizwa kwa sababu baadhi yetu ambao bado tuna kesi tuna kiwewe.

Idrissa Sylvaine ni Mshauri wa haki sheria wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) anasema, “Tathmini hiyo itasaidia kukuza utawala wa sheria, kuleta haki kwa waathiriwa na kuwawajibisha askari wa SSPDF. Tathmini hiyo pia itachangia katika mchakato wa amani nchini Sudan Kusini.”