Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunahitaji mshikamano wa kimataifa sasa kuliko wakati mwingine wowote Guterres auambia mkutano wa CELAC

Katibu Mkuu António Guterres (kushoto) akitoa hotuba kwenye Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Jumuiya ya Nchi za Amerika Kusini na Caribbea (CELAC) huko Saint Vincent na Grenadines.
UN Photo/Lucanus Ollivierre
Katibu Mkuu António Guterres (kushoto) akitoa hotuba kwenye Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Jumuiya ya Nchi za Amerika Kusini na Caribbea (CELAC) huko Saint Vincent na Grenadines.

Tunahitaji mshikamano wa kimataifa sasa kuliko wakati mwingine wowote Guterres auambia mkutano wa CELAC

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo ameueleza mkutano wa nane wa jamii za nchi za Amerika Kusini na Caribbea, CELAC kwamba Dunia hivi sasa inahitaji mshikano wa hali ya juu kuliko wakati mwingine wowote.

Katika mkutano huo unaofanyika kwenye visiwa na  Saint Vincent and Grenada pia amekipongeza kisiwa cha Saint Vincent kwa mnepo mkubwa kilichouonyesha baada ya kukumbwa na mlipuko wa volkano.

Guterres ambaye amegusia mada mbalimbali katika mkutano huo. Akizungumzia amani na usalama ametambua hatua kubwa zilizopigwa  katika mchakato wa Amani Colombia na mazunumzo baina ya Guyana na Venezuela katika nchi la Amerika Kusini.

Changamoto ya uhalifu

Katibu Mkuu pia amegusia changamoto kubwa ya uhalifu wa kikatili, usafirishaji haramu wa silaha na changamoto za usalama zinazokabili mataifa ya Ecuador, Guatemala, na Haiti na kutoa wito wa ushirikiano wa kimataifa kukabiliana na tishio la usalama kwa ufanisi.

Amesema “Nchini Haiti, hali ambayo tayari ni mbaya inazidi kuwa mbaya siku hadi siku. Magenge ya uhalifu yanaishikilia nchi hiyo na kutumia unyanyasaji wa kingono kama silaha. Wakati huo huo, Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kukabiliana na changamoto za kibinadamu Haiti unahitaji usaidizi thabiti wa kifedha”.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (kulia) akihudhuria Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Jumuiya ya Nchi za Amerika Kusini na Caribbea (CELAC) huko St. Vincent na Grenadines.
UN Photo/Lucanus Ollivierre

Malengo ya maendeleo endelevu

Akizungumza kuhusu mshikamano kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu Guterres ametoa wito wa msaada wa kifedha, msamaha wa madeni, na ufadhili wa masharti nafuu kwa nchi zilizo hatarini zaidi.

Amechagiza kuhusu kichocheo cha malengo ya SDG na kurekebisha usanifu wa mifumo ya kifedha ya kimataifa.

Pia Katibu Mkuu “ameangazia changamoto za kimataifa za ubabe, msimamo mkali, habari potofu, na kuongezeka kwa ukosefu wa usawa.“

António Guterres amesisitiza  kusuhu tishio linaloletwa kwa mataifa ya visiwa vidogo vinavyoendelea kutokana na dharura ya mabadiliko ya tabianchi akisema wakati wa kuchukua hatua kuepusha zahma kubwa ni sasa.

Maeneo manne ya kuyapa kipuambele

Guterres ameuambia mkutano huo kwamba mnapokusanyika ili kusaidia kusaka suluhu kwa eneo lenu na kwa ulimwengu ningependa kuangazia maeneo manne muhimu

Mosi: tunahitaji mshikamano kwa ajili ya amani na usalama.

Amesema Amerika ya Kusini na Caribbea zimeonyesha jinsi gani kuungana kwa ajili ya amani kunawezekana na kuleta mabadiliko. 

Tumeshuhudia hivi leo “Mchakato wa amani nchini Colombia umepiga hatua kubwa, na mchango wa thamani kutoka kwa nchi za CELAC.”

Ameendelea kusema kuwa Tamko la Pamoja la mazungumzo ya amani kati ya Guyana na Venezuela, lililopitishwa hapa Argyle Desemba mwaka jana, ni mfano mwingine wa kujitolea kwa eneo hilo kutafuta suluhu za amani, na ninapongeza juhudi zenu”.

Lakiniamesema kesi zote mbili pia zinasisitiza kwamba utekelezaji unahitaji juhudi endelevu.

Na pia tunajua kuwa amani ni zaidi ya kutokuwepo kwa migogoro ya silaha. Leo, uhalifu wa kikatili na uliopangwa unaendelea kusumbua nchi nyingi. Ulanguzi wa silaha umekuwa tishio kubwa zaidi la usalama kwa kanda. Haitawezekana kupambana kwa ufanisi bila ushirikiano wa kimataifa wenye nguvu zaidi  kuanzia kwenye chanzo hadi mitaani.” 

Pili: tunahitaji mshikamano kwa maendeleo endelevu.

Katibu Mkuu ameonya kwamba Malengo ya Maendeleo Endelevu yanakwenda kombo. Mamilioni ya watu katika eneo hilo wanakabiliwa na umaskini na njaa.

Amesema “Ninakaribisha Mpango wenu wa hivi karibuni wa uhakika wa chakula na lishe na kutokomeza njaa kufikia 2030. Lakini hiyo inahitaji ufadhili na nchi nyingi tayari zinazama katika madeni.”

Ameongeza kuwa mfumo wa kifedha wa kimataifa unashindwa kutoa ufadhili wa muda mrefu kwa nchi zinazohitaji na kutoa ulinzi wa kijamii wa kifedha duniani.

Na hilo amesema “Nchi Zinazoendelea za Visiwa Vidogo zimeathirika zaidi.”

Amesisitiza kuwa “Nchi za kipato cha kati pia hazipati msaada wanaohitaji. Licha ya udhaifu wao, hawapati manufaa ya msamaha muhimu wa madeni na ufadhili wa masharti nafuu. Hii lazima ibadilike. Hiyo inaonyesha umuhimu wa kupitishwa kwa faharasa ya mazingira magumu.”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (kulia) akihudhuria Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Jumuiya ya Nchi za Amerika Kusini na Caribbea (CELAC) huko St. Vincent na Grenadines.
UN Photo/Lucanus Ollivierre
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (kulia) akihudhuria Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Jumuiya ya Nchi za Amerika Kusini na Caribbea (CELAC) huko St. Vincent na Grenadines.

Tatu: tunahitaji mshikamano kwa umoja wa kijamii.

Guterres amesema Ulimwenguni kote, ubabe na misimamo mikali inaongezeka. Demokrasia na nafasi za kiraia zinamomonyoka. Taarifa potofu na kauli za chuki zimechangiwa zaidi na teknolojia mpya na ukosefu wa usawa unaoongezeka unaleta hofu za watu.

Uhamaji usio wa kawaida umekuwa chombo cha kisiasa cha kuleta mgawanyiko na ni muhimu sana kushughulikia sababu zote ambazo zimebadilisha hili kuwa tatizo kubwa kwa bara hili.

Guterres amesema “Ninatoa wito wa mkataba mpya wa kijamii, unaozingatia uaminifu, haki na ushirikishwaji na unaozingatia haki za binadamu katika nyanja zake zote.”

Kwani amesema  “Viongozi wana wajibu wa kuwekeza katika mshikamano wa kijamii, kukomesha ukatili na ubaguzi, kulinda haki za wenye asili ya Afrika na wenyeji na kuhakikisha kuwa kila jamii inahisi kuwakilishwa na kujumuishwa ili kuhakikisha ushiriki kamili wa wanawake na uongozi na kukuza sauti za vijana.”

Nne: tunahitaji mshikamano kushughulikia dharura ya mabadiliko ya tabianchi 

Katibu mkuu amehitimisha tarifa yake kwa kusema Dunia inahitaji mshikano kwa kushughulikia dharira ya mabadiliko ya tabianchi ambayo inatishia kutoweka kwa visiwa vidogo vinavyoendelea.

Amesema matukio makubwa yanazidi kuongezeka na kwamba “Nchi zote lazima zijitolee kwa michango mipya iliyoamuliwa kitaifa kwa uchumi mzima ifikapo mwaka 2025 ambayo inakwenda sanjari na kupunguza viwango vya joto duniani hadi nyuzi joto 1.5.”

Amesisitiza kuwa mipango hii inapaswa kutumika kama mipango ya mpito na uwekezaji. 

“Nchi za mataifa tajiri za G20 zinazohusika na asilimia 80 ya uchafuzi wa hewa duniani zina wajibu maalum wa kuongoza juhudi hizi.” Amesema Guterres

Na kuongeza kuwa ni lazima ziongoze hatua za kimataifa za kuondoa mafuta ya kisukuku na kuharakisha mpito wa haki na wa usawa kwa vitu vinavyoweza kurejelezwa.

“Najua nchi nyingi zimeanzisha nishati mbadala iliyogatuliwa. Lakini zinahitaji msaada. Tunahitaji nchi zilizoendelea kutoa haki ya kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabianchi kwa kulipa sehemu yao waliyoahidi.”