Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA yazitaka pande zinazohasimiana Sudan Kulinda raia na kukomesha mapigano mara moja

Watoto na familia za Sudan zilizofurushwa kutoka Gezira zakimbia kwa miguu baada ya mapigano kuzuka Wad Madani, jimbo la Al Jazirah.
© UNICEF/Proscovia Nakibuuka
Watoto na familia za Sudan zilizofurushwa kutoka Gezira zakimbia kwa miguu baada ya mapigano kuzuka Wad Madani, jimbo la Al Jazirah.

OCHA yazitaka pande zinazohasimiana Sudan Kulinda raia na kukomesha mapigano mara moja

Msaada wa Kibinadamu

Takriban miezi tisa ya vita imeifanya nchi ya Sudan kutumbukia katika hali duni ambayo inazidi kuwa mbaya siku hadi siku, wakati mzozo unapoenea, mateso ya wanadamu yanazidi kuongezeka, ufikishaji wa misaada ya kibinadamu nao unapungua, na matumaini yanapungua, lakini hali hii haiwezi kuendelea.

Hayo yapo kwenye taarifa iliyotolewa hii leo mjini New York Marekani na Martin Griffiths, Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, ambapo amesema mwaka 2024 jumuiya za kimataifa hasa zile zenye ushawishi kwa wahusika katika mzozo nchini Sudan wachukua hatua madhubuti na za haraka kusitisha mapigano na kulinda operesheni za kibinadamu zinazolenga kusaidia mamilioni ya raia.

Ukiukwaji wa haki za binadamu

Kwa mujibu wa Griffiths, katika Jimbo la Aj Jazirah, kuna hatari, zaidi ya watu 500,000 wamekimbia mapigano ndani na karibu na mji mkuu wa jimbo la Wad Medani, eneo ambalo kwa muda mrefu limekuwa kimbilio kwa wale walioyakimbia makazi yao kutokana na mapigano sehemu nyingine, uhamisho wa watu wengi unaoendelea na unaweza kuchochea kuenea kwa haraka kwa mlipuko wa kipindupindu katika jimbo hilo, huku zaidi ya watu 1,800 wakishukiwa kuwa na ugonjwa huo hadi sasa.

Unyanyasaji wa kutisha ambao umefafanua vita hivi katika maeneo yenye joto kama Jimbo la Khartoum, Darfur na Kordofan, sasa unaripotiwa huko Wad Medani, taarifa za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia, zinakumbusha kwamba wahusika katika mzozo huu bado wanashindwa kutekeleza ahadi zao za kulinda raia.

Kuna wasiwasi mkubwa kuhusu kufuatwa kwa sheria za kimataifa za Kibinadamu, kwa kuzingatia umuhimu wa Wad Medani kama kitovu cha shughuli za misaada, “mapigano huko na uporaji wa maghala na vifaa vya kibinadamu ni pigo kubwa katika juhudi zetu za kutoa chakula, maji, huduma za afya, na misaada mingine muhimu”. Amesema mkuu huyo wa OCHA.

Griffiths ameongeza kuwa “ninaukemea vikali uporaji wa misaada ya kibinadamu, ambao unadhoofisha uwezo wetu wa kuokoa maisha”.

Watoto na familia wakikimbia kwa miguu kutoka Wad Madani, jimbo la Al Jazirah kufuatia mapigano ya hivi karibuni.
© UNICEF/UNI492302/Mohamdeen
Watoto na familia wakikimbia kwa miguu kutoka Wad Madani, jimbo la Al Jazirah kufuatia mapigano ya hivi karibuni.

Mambo matatu yashughulikiwe

 Ghasia zinazoongezeka nchini Sudan pia zinahatarisha utulivu wa kikanda, vita hivyo vimeibua mzozo mkubwa zaidi wa watu waliokimbia makazi yao, na kung'oa maisha ya zaidi ya watu milioni 7, wengine milioni 1.4 kati yao wamevuka hadi nchi jirani ambazo tayari zina idadi kubwa ya wakimbizi.

Kwa watu wa Sudan, mwaka 2023 ulikuwa mwaka wa mateso, na kinachotazamiwa ni kwamba 2024, wahusika katika mzozo lazima wafanye mambo matatu kuumaliza: Kulinda raia, kuwezesha ufikiaji wa kibinadamu, na kukomesha mapigano mara moja.

Msaada wa kibinadamu

Nchini Sudan, karibu watu milioni 25 watahitaji usaidizi wa kibinadamu mwaka 2024, lakini ukweli mbaya ni kwamba kuongezeka kwa uhasama kuna waweka wengi wao nje ya uwezo wa kupatiwa usaidizi wa kibinadamu amesema mkuu huyo wa OCHA.

“Usafirishaji katika mstari wa mapigano umesimama, ingawa operesheni ya misaada kutoka Chad kupitia mpaka inaendelea kuwa mkombozi kwa watu Darfur, juhudi za kusambaza misaada mahali pengine zinazidi kuwa hatarini”.