Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVID-19 na machafuko vimezidisha matatizo ya akili Ukraine:WHO

Wataalamu wa kisaikolojia wanawasadia mabinti wali katika mazingira hatarishi kaskazini mwa Ukraine wakati huu ambapo kuna vuzizi kutokana na janga la COVID-19 ambavyo vinawaathiri afya ya akili.
© UNICEF/Aleksey Filippov
Wataalamu wa kisaikolojia wanawasadia mabinti wali katika mazingira hatarishi kaskazini mwa Ukraine wakati huu ambapo kuna vuzizi kutokana na janga la COVID-19 ambavyo vinawaathiri afya ya akili.

COVID-19 na machafuko vimezidisha matatizo ya akili Ukraine:WHO

Afya

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limesema janga la corona au COVID-19 na vita vya muda mrefu vimesababisha athari kubwa ya matatizo ya afya ya akili nchini Ukaraine na kuongeza pengo la kupata huduma kwa waathirika. Jason Nyakundi na taarifa zaidi 

Katika eneo la Slovianski Ukraine timu ya wataalam wa mradi maalum wa WHO kwa ajili ya huduma ya afya ya akili wanaanza safari ndefu ya kupita nyumba kwa nyumba kwenda kuwatembelea na kuwasaidia watu na familia zilizoathirika na matatizo ya akili. 

Team hiyo ipo chini ya mradi ambao WHO iliamua kuuanzisha kutokana na ongezeko kubwa la watu wanaokabiliwa matatizo ya afya ya akili na wanashindwa kupata au kufikia huduma kutokana na vita vinavyoendelea nchini humo lakini pia janga la COVID-19.  

Oleksii Kostychenko ni mmoja wa wataalam hao anasema “Kuna idadi kubwa sana ya watu wenye matatizo ya akili, wengi wakikabiliwa na wasiwasi, wazimu na msongo wa mawazo, inaonekana kwamba kiwango cha tatizo hili  kimeongezeka sana baada ya vita kuzuka. Na kwa ujumla, watu wote ambao walitujia wakiwa na matatizo ya kuwa na hofu na wasiwasi, walikuwa wengi sana, na asilimia 99 kati yao wamepitia na kushuhudia vita vya kijeshi, kwa hivyo hii imekuwa na athari kubwa sana katika jamii. " 

Timu yao ina jumla ya wataalam saba wanaojumuisha mtaalamu wa magonjwa ya akili, mwanasaikolojia, muuguzi na mfanyakazi wa kijamii. Na timu hii husafiri hadi maeneo ya ndani vijijini kufikisha huduma. 

wataalamu hao waliwasili nyumbani kwa Natalia Sergun mmoja wa wanufaika wa mradi huu ambaye amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya akili kwa muda sasa. Anaishi Bylbasivka na watoto wake watatu pamoja na kaka yake. “Vita vimeathiri sana afya yangu lakini pia vinaathiri maisha yangu, kwani madirisha ya nyumba yangu yalipasuka baada ya bomu kulipuka, kisha moto ukatekeketeza kabisa nyumba yangu na baada ya hapo mwanangu aliyekuwa akiishi na ulemavu akafariki dunia akiwa na umri wa miaka 2. Yote haya ymeaniathiri vibaya kiakili, nilikuwa bado namuomboleza mwanangu ikanibidi nilazwe kwenye hospitali ya matatizo ya akili.” 

Kwa sasa Natalia amepata ahuweni na anaishi na wanawe bila shida akiendelea kupata matibabu na huduma na anatoa asante kwa mradi wa WHO wa kusaidia matatizo ya afya ya akili kwani anasema la sivyo angekuwa bado kwenye wodi ya wendawazimu hospitali.