Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vizuizi Gaza vyaacha asilimia 80 ya wakazi wake wakitegemea msaada wa kigeni- UNCTAD.

Huko Gaza, msichana mdogo anakula mkate ambao mama yake alitengeza kutoka kwa bidhaa zilizonunuliwa na pesa taslim inayosambaswa na WFP.
© WFP/Mostafa Ghroz
Huko Gaza, msichana mdogo anakula mkate ambao mama yake alitengeza kutoka kwa bidhaa zilizonunuliwa na pesa taslim inayosambaswa na WFP.

Vizuizi Gaza vyaacha asilimia 80 ya wakazi wake wakitegemea msaada wa kigeni- UNCTAD.

Ukuaji wa Kiuchumi
  • Mfumuko wa bei 
  • Fursa za kujipatia kipato zazidi kupungua 
  • Misaada ya kigeni yapungua 
  • Asilimia 80 ya wakazi wa Gaza ni wategemezi 

Mwaka 2022 ulikuwa ni mwaka mwingine mbaya kwa wapalestina wanaoishi Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati, imesema ripoti ya hivi punde zaidi ya Kamati ya Biashara na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD

Ripoti hiyo kuhusu usaidizi wa UNCTAD kwa wapalestina iliyozinduliwa leo huko jijini Geneva, Uswisi inasema hata kabla ya mzozo wa sasa, mzingiro wa miongo kadhaa wa Gaza  uliathiri uchumi wa eneo hilo linalokaliwa kimabavu na Israeli na kuacha asilimia 80 ya wakazi wake wakitegemea misaada kutoka nje. 

Hii ni kwa vile mfumuko wa bei ya bidhaa, kupungua kwa fursa za kujipatia kipato, kupungua kwa misaada ya kigeni na kuongezeka kwa deni kuliweka uchumi wa eneo hili chini ya kiwango chake cha uchumi kabla ya janga COVID-19

Ripoti inaangazia mazingira yaliyowekwa ya kuhakikisha uchumi wa Palestina unategemea Israeli, ambapo gharama za ziada za uzalishaji na miamala, halikadhalika vikwazo vya biashara na maeneo mengine ya dunia, vimefanya nakisi ya biashara na utegemezi kwa Israeli, kwani kwa mwaka 2022 asilimia 72 ya biashara Palestina ilikuwa na Israeli. 

Ukosefu wa ajira nao umesalia kiwango cha juu cha asilimia 24 kwenye eneo linalokaliwa la wapalestina, asilimia 13 Ukingo wa Magharibi na asilimia 45 Gaza ambapo walioathiriwa zaidi ni wanawake na vijana. Umaskini umekithiri na wakazi wanahitaji misaada ya kibinadamu. 

UNCTAD inasema miongo mitatu baada ya mikataba miwili ya Oslo kati ya Israeli na Palestina, matumaini ya kwenda sambamba kwa uchumi wa Israeli na Palestina yanazidi kukumbwa na vikwazo vinavyotokana na será za vizuizi, pato la ndani la Palestina kwa sasa likiwa ni 8% tu chini ya pato la ndani ya taifa la Israeli. 

Soma ripoti zaidi hapa.