Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madai halali hayawezi kuhalalisha ugaidi, na ugaidi hauwezi kuhalalisha adhabu ya pamoja: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (Kushoto) na waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Hassan Shoukry Selim mjini Cairo
UN Photo/Eskinder Debebe

Msaada wa Kibinadamu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye yuko Cairo Misri  amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje w anchi hiyo Sameh Shoukry na kisha kuzungumza kwa pamoja na na waandishi wa habari akisema yuko ziarani Mashariki ya Kati kuona misaada ya kibinadamu inayohitajika inawasilishwa kwa wahitaji huko Ukanda wa Gaza kupitia kivuko cha Rafah. 

Tweet URL

Amesema amefanya hivyo katika wakati wa mgogoro mkubwa na tofauti kuwahi kushuhudiwa katika Ukanda mzima kwa miongo kadhaa.

Katibu Mkuu amesema anatammbua na kumpongeza Rais Abdel Fattah Al sisi wa Misri kwa uongozi wake.

Mmkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema mgogoro huu ulisababishwa na mashambulizi mabaya ya Oktoba 7 ya Hamas ambayo yaliua, kujeruhi na kuteka nyara idadi kubwa ya raia kutoka Israeli, na pia kutoka duniani kote.

Na hii ilipelekea Israel kuzingira kabisa Gaza na kuendesha kampeni isiyokoma ya ya kurusha makombora, na kuongeza madhila kwa idadi kubwa ya raia ambao wengi wao ni wanawake na watoto, lakini pia waandishi wa habari, wafanyakazi na wengine wengi, wakiwemo wafanyakazi wetu wenyewe wa Umoja wa Mataifa.

Sheria za kibinadamu za kimataifa lazima zizingatiwe

Guterres amesisitiza kwamba “Niseme wazi kabisa, nikisisitiza tena kwamba sheria za kimataifa za kibinadamu lazima ziheshimiwe, na kwamba ulinzi wa raia pia ni lazima, na mashambulizi yoyote kwenye hospitali, shule au majengo ya Umoja wa Mataifa ni marufuku chini ya sheria za kimataifa.”

 Ameongeza kuwa “Katika kukabiliana na janga hili la kibinadamu, naomba hatua mbili za haraka za kibinadamu zichukuliwe, kwa Hamas kwa ajili ya kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa mateka wote na kwa Israeli, kutoa fursa ya haraka na ya bila vikwazo ya kufikisha misaada ya kibinadamu, ili kukabiliana na mahitaji ya msingi zaidi ya watu wa Gaza.”

Hakuna kinachohalalisha mashambulizi 

Bwana Guterres ameweka bayana kwamba  “Watu wa Palestina wana malalamiko ya halali na mazito baada ya miaka 56 ya kukaliwa kwa mabavu. Lakini kama yalivyo mazito malalamiko hayo, hayawezi kuhalalisha mashambulizi ya kigaidi na hii ya kutisha kama hivi. Lakini vivyo hivyo mashambulizi haya hayawezi kuhalalisha adhabu ya pamoja ya watu wa Palestina.”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Antonio Guterres akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Misri katika mkutanona waandishi wa habari mjini Cairo
UN Photo/Eskinder Debebe
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Antonio Guterres akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Misri katika mkutanona waandishi wa habari mjini Cairo

Sheria za kibinadamu za kimataifa lazima zizingatiwe

Guterres amesisitiza kwamba “Niseme wazi kabisa, nikisisitiza tena kwamba sheria za kimataifa za kibinadamu lazima ziheshimiwe, na kwamba ulinzi wa raia pia ni lazima, na mashambulizi yoyote kwenye hospitali, shule au majengo ya Umoja wa Mataifa ni marufuku chini ya sheria za kimataifa.”

 Ameongeza kuwa “Katika kukabiliana na janga hili la kibinadamu, naomba hatua mbili za haraka za kibinadamu zichukuliwe, kwa Hamas kwa ajili ya kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa mateka wote na kwa Israeli, kutoa fursa ya haraka na ya bila vikwazo ya kufikisha misaada ya kibinadamu, ili kukabiliana na mahitaji ya msingi zaidi ya watu wa Gaza.”

Majengo yaliyosambaratishwa Al-Kass Gaza
© WFP
Majengo yaliyosambaratishwa Al-Kass Gaza

Mapigano lazima yakome sasa

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa “Maombi yangu yote mawili ya kibinadamu ni muhimu, na ili kusaidia kutimiza maombi haya mawili natoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja kwa ajili ya masuala ya kibinadamu.”

Amesema kwa takriban wiki mbili, watu wa Gaza wameishi bila msaada wowote yote ya msaada wa chakula, maji, dawa na vitu vingine muhimu. Magonjwa yanaenea na vifaa vinapungua.

“Watu wanakufa na nimeshitushwa sana na picha za vifo na uharibifu katika hospitali ya Al-Ahli. Raia wa Gaza wanahitaji sana huduma na vifaa vya msingi, na kwa hilo tunahitaji fursa ya haraka ya ufikiaji usiozuiliwa thomas misaada ya  kibinadamu.”

Misaada inapaswa kuwa endelevu

Katibu Mkuu amesema Pamoja na misaada ya chakula, maji, dawa na mafuta, sasa tunahitaji misaada hiyo kwa kiwango kikubwa na tunahitaji kuwa endelevu.Sio operesheni moja ndogo ambayo inahitajika. Ni juhudi endelevu za kufikisha misaada ya kibinadamu kwa watu wa Gaza.

Kwa maneno mengine amesema Guterres, hiyo ina maana kwamba wahudumu wa kibinadamu wanahitaji kuweza kupata msaada huo, na wanahitaji kuwa na uwezo wa kuusambaza kwa usalama. 

Amemalizia kwa kusema “Niko Misri kushuhudia matayarisho ya Umoja wa Mataifa ili kuweza kutoa msaada mkubwa kwa watu wa Gaza katika juhudi hizi za kuokoa maisha, uwanja wa ndege wa El-Arish na kivuko cha Rafah sio muhimu tu, ni tumaini letu pekee. Hiyo ndio njia ya maisha kwa watu wa Gaza.”

Kesho Ijumaa Guterres atazuru uwanja wa ndege wa Al-Arish, kituo cha Umoja wa Mataifa cha masuala ya kiufundi na kivuko cha mpaka wa Rafah na Jumamosi atakutana na Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi