Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoka Melbourne Australia hadi New York, kutumia muziki kueneza ujumbe wa matumaini

Kwaya ya wahudumu wa afya ya hospitali ya kifalme ya Melbourne nchini Australia wakiwa na Rana Sidani (katikati) Mshauri wa WHO,
UN/Assumpta Massoi
Kwaya ya wahudumu wa afya ya hospitali ya kifalme ya Melbourne nchini Australia wakiwa na Rana Sidani (katikati) Mshauri wa WHO,

Kutoka Melbourne Australia hadi New York, kutumia muziki kueneza ujumbe wa matumaini

Afya

Sauti za wanakwaya zinasikika kwenye milango ya kuingia jengo la makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani na ni ya wanakwaya wahudumu wa afya wakiwemo madaktari wa hospitali ya kifalme ya Melbourne nchini Australia.

Wanakwaya hao wanne, wanawake watatu na mwanaume mmoja wameletwa mahsusi na shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO kuchagiza nafasi ya muziki katika tiba hususan afya ya akili.

Flora Nducha wa Idhaa hii ya  Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alizungumza na Rana Sidani, Mshauri wa WHO kutoka Geneva, Uswisi na kueleza kuwa uwepo wa kwaya hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 75 ya shirika hilo la afya mwaka huu wa 2023.

Amesema kupitia nyimbo hizo, wanakwaya hao wanaeneza ujumbe wa matumaini pia hasa wakati huu ambapo malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yanakumbwa na mkwamo kutokana na changamoto mbali mbali, lakini watu wajue kuwa lipo tumaini la kuweza kufanikisha iwapo kila mtu atatekeleza wajibu wake.

Waimbaji  hawa ni wahudumu wa afya na wanaamini katika nguvu ya muziki katika afya ya akili, amesisitiza Bi. Sidani.