Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajali za Meli Nigeria na Ugiriki, UN yatoa neno

Wahamiaji wanaokolewa katika pwani ya Libya na NGO, SOS Méditerranée. (file)
© SOS Méditerranée/Anthony Jean
Wahamiaji wanaokolewa katika pwani ya Libya na NGO, SOS Méditerranée. (file)

Ajali za Meli Nigeria na Ugiriki, UN yatoa neno

Wahamiaji na Wakimbizi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameshtushwa na taarifa za meli iliyokuwa imebeba watu takriban 400 kupinduka karibu na fukwe ya Pylos, nchini Ugiriki na kupoteza maisha ya wanawake, wanaume na watoto.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric akizungumza na waandishi wa habari hii leo jijini New York Marekani amesema mpaka sasa kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM, watu 104 wamefanikiwa kuokolewa huku wengine 32 miili yao imeopolewa.

Juhudi za uokoaji zinaendelea ingawa wasiwasi mkubwa wa IOM ni kuwa watu wengi wanahisiwa kupoteza maisha.

Wengi wa watu hao waliokuwa kwenye meli hiyo wanahisiwa kuwa ni wahamiaji.

“Katibu Mkuu Guterres amekumbusha na kusisitiza wito wake kwamaba kila mtu anayetafuta maisha bora anahitaji utu na usalama. Huu ni mfano mwingine wa hitaji la nchi Wanachama kukusanyika pamoja na kuunda njia salama kwa watu wanaolazimika kukimbia nchi zao na kuchukua hatua za kina kuokoa maisha baharini na kupunguza safari hatari.” Amesema Dujarric

https://twitter.com/UNmigration/status/1668922182347501569

Ajali ya meli Nigeria

Wakati huo huo Msemaji huyo wa Umoja wa Mataifa  amesema nchini Nigeria nako kumetoa ajali ya meli ambapo meli imezama na watu kupoteza maisha.