Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sema “asante mama” kwa kuchukua hatua kuokoa maisha ya akina mama- UNFPA

Kupata haki za akina mama tunahitaji kupata kwanza usawa wa kijinsia
© UNFPA/ARTificial Mind/Cecilie Waagner Falkenstrøm
Kupata haki za akina mama tunahitaji kupata kwanza usawa wa kijinsia

Sema “asante mama” kwa kuchukua hatua kuokoa maisha ya akina mama- UNFPA

Wanawake

Kwa akina mama wengi duniani kote, mwezi wa Mei ni tukio la kila mwaka kwa wao kupokea shukrani na kutambuliwa kwa kile wakifanyacho, inasema makala iliyochapishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya watu duniani kuadhimisha siku ya mama duniani tarehe 14 mwezi Mei..

Ingawa hivyo, kwa maelfu ya akina mama wengi duniani kote, kutambuliwa huko kunaenda mbali sana. Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni zaidi, mwanamke mmoja anafariki dunia kutokana na ujauzito au wakati akijifungua kila baada ya sekunde mbili – kiwango kikubwa cha vifo hivi vinatokana na sababu zinazoweza kuzuilika kama vile kuvuja damu na maambukizi.

Kitu kibaya zaidi ni kwamba, majawabu ya matatizo haya yamekuweko kwa miongo kadhaa; lakini yanahitaji uwekezaji wa haraka kwenye uzazi wa mpango na kwa dunia kupatia jawabu uhaba mkubwa wa wakunga, ambao kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya watu, UNFPA, inasema wanaweza kuzuia takribani theluthi mbili ya vifo vya wajawazito na watoto wachanga duniani.

“Mbinu tunazo, ufahamu, halikadhalika rasilimani za kutokomeza vifo vinavyozuilika vya wajawazito; kile ambacho tunahitaji sasa hivi ni ni utashi wa kisiasa,” anasema Dkt. Natalia Kanem Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA kupitia taarifa.

Vifo vya wajawazito viko katika kiwango cha juu – na hali inazidi kuwa mbaya

Kati ya mwaka 2000 na 2015, vifo vya wajawazito duniani vilipungua kwa zaidi ya theluthi moja. Lakini kiwango cha kupungua kimekwama katika kanda zote duniani na hata kwingineko maendeleo yaliyopatikana yanarudi nyuma.

"Haikubaliki kwamba wanawake wengi bado wanaendelea kufariki dunia wakati wa ujauzito na kujifungua. Zaidi ya vifo 280,000 kwa mwaka mmoja haikubaliki,” amesema Dkt. Kanem akiongeza “Tunaweza na tunapaswa tufanye vema zaidi.”

Mara nyingi, suala la kuwa mama si jambo la kuchagua

Mara nyingi na kama si hivyo, wanawake na wasichana hawana uamuzi kuhusu kubeba ujauzito.

Wanawake wanne kati ya 10 waliokuwa kwenye uhusiano hawakuwa na uwezo wa kuamua iwapo atumie njia ya mpango wa uzazi, apate huduma ya afya au kujamiiana au la, na hii ni katika nchi 68. Wakati  huo huo, takwimu zinadokeza kwamba ujauzito utokanao na kubakwa hutokea mara kwa mara kama ilivyo kwa ujauzito unaopatikana baada ya maridhiano ya kujamiiana.

Vigezo hivi na vinginevyo vinachochea janga la dunia lililosahaulika, ambamo kwalo nusu ya ujauzito duniani kote ni ile ambayo haikupangwa, na hivyo kuleta madhara kwa wale wote wahusika.

Mara nyingi, chaguo la kuwa mama si chaguo kabisa, mara nyingi mwanamke hawezi kuchagua na kuamua.
© UNFPA/ARTificial Mind/Cecilie Waagner Falkenstrøm
Mara nyingi, chaguo la kuwa mama si chaguo kabisa, mara nyingi mwanamke hawezi kuchagua na kuamua.

Kama ilivyotajwa, changamoto wakati wa ujauzito na kujifungua hasa kwa barubaru wa kike na wasichana. Takribani vizazi 500,000 vilikuwa kwa wasichana wenye umri wa kati ya miaka 10 hadi 14 mwaka 2021, na hivyo kufanya mamia ya maelfu ya akina mama ilhali bado ni watoto.

“Idadi hii kubwa ya mimba zisizopangwa inawakilisha kushindwa kwa harakati za kimataifa za kulinda haki za msingi za wanawake na watoto wa kike,” amesema Mkurungezi Mtendaji wa UNFPA Dkt. Natalia Kanem.

Chaguo la mwanamke kuhusu uzazi mara nyingi hupuuzwa

Mwezi Novemba mwaka 2022, Idadi ya watu duniani ilifikia bilioni 8. Wakati wengi walipokea taarifa hizi kwa bashasha kwa kuwa hatua hii inatokana na kuboreshwa kwa huduma za afya na kupunguza umaskini, wengine wanasugua mikono yao wakiwaza na kuwazua iweje “kuna watu wengi” au “watu wachache” duniani.

Fikra hizi zinaweza miili ya wanawake kwenye sehemu ya kuwa majawabu kwenye changamoto za ongezeko la idadi ya watu – hili ni wazo  hatarishi.

Kihistoria, fikra hizi zimesababisha kuweko kwa sera kali zilizoumbwa kudhibiti suala la uzazi wa mwanamke, jambo ambalo linahatarisha haki zao huku likikandamiza matamanio yao.

Kwa mujibu wa ripoti ya UNFPA ya hali ya watu duniani mwaka huu wa 2023, wanawake wengi wanataka familia familia kubwa au ndogo kuliko ile waipatayo.

Katika nchi zote za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara, mathalani, wanawake wanaripoti kuwa na watoto wawili au zaidi kuliko watakavyo, ilhali wanawake wasio na watoto Japan walisema wao wanataka watoto.

Zaidi ya hayo, katika nchi za vipato vya chini na kati, mwanamke 1 kati ya 4 wanafikia matamanio yao ya uzazi.

Kile ambacho wanawake na akina mama wanataka pindi linapokuja suala la uzazi ni jambo la kuzingatiwa. Lakini kwa bahati mbaya, mara nyingi hakuna anayeuliza.

Kurejesha haki za akina mama, tunahitaji kurejesha usawa jinsia

Kuzuia vifo vya wajawazito, kunyima haki vyote hivyo vinaweza kubadilishwa kwa kufanya dunia kuwa pahala pa usawa kwa watu wa jinsia zote.

Bila shaka, ni rahisi kusema kuliko kutekeleza. Lakini mchango wa ukosefu wa usawa wa kijinsia katika mizizo ya masuala mengi ikiwemo yaliyotajwa hapo juu lazima utambuliwe.

Ukosefu wa usawa wa kijinsia ndio kinafanya wanawake wengi wasiwe kwenye nguvukazi, shuleni, wawe hatarini kwenye mizozo, ghasia na kunyimwa haki ya kupitisha uamuzi wa masuala yanayowahusu ikiwemo miiili na afya zao. Na hicho ndio kinafanya ujauzito kuwa hatarishi, kitu ambacho mamia ya wanawake wanakufa.

Siku hii ya Mama duniani, ina maana pale unaposema asante kwa akina mama kwenye maisha yao kwa kuchukua hatua kuokoa maisha yao. Nao watakushukuru kwa ubora zaidi.