Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yalani ubaguzi kwa baadhi ya watu wanaokimbia Ukraine

Wakimbizi kutoka Ukraine wakiingia nchini Poland katika mpaka wa Medyka.
© UNHCR/Chris Melzer
Wakimbizi kutoka Ukraine wakiingia nchini Poland katika mpaka wa Medyka.

UNHCR yalani ubaguzi kwa baadhi ya watu wanaokimbia Ukraine

Wahamiaji na Wakimbizi

Kamishna mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, leo amezungumza  dhidi ya hali mbaya kuhusu baadhi ya wakimbizi wanaokimbia kuvuka mpaka wa Ukraine, na raia wa nchi ya tatu, kwamba wamekuwa wakikabiliwa na ubaguzi wa rangi na ubaguzi mwingine. 

Katika taarifa iliyotolewa kuadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza ubaguzi wa rangi, Filippo Grandi amesema ingawa ameguswa na uungwaji mkono unaoonekana kutoka kwa jamii zinazowakaribisha zaidi ya wakimbizi milioni tatu wa Ukraine tangu mashambulio kutoa Urusi yaanze, watu wengi walio wachache  mara nyingi wageni ambao walikuwa wakisoma au kufanya kazi huko wameelezea uzoefu tofauti sana. 

Taarifa hiyo ikimnukuu bwana Grandi imesema, "Pia tulishuhudia hali mbaya, kwamba baadhi ya watu weusi na kahawia wanaokimbia Ukraine na vita vingine na migogoro duniani kote  hawajapata kutendewa sawa na wakimbizi wa Ukraine". 

Ubaguzi usiokubalika 

Kamishna mkuu huyo amesema kwamba, "Waliripoti matukio ya kutatanisha ya ubaguzi, vurugu, na ubaguzi wa rangi. Vitendo hivi vya ubaguzi havikubaliki, na tunatumia njia na rasilimali zetu nyingi kuhakikisha kwamba watu wote wanalindwa kwa usawa.” 

Mkuu huyo wa UNHCR ametanabaisha kwamba uzoefu wa wakimbizi ulimwenguni kote ni sawa, wenye “maumivu na huzuni sawa, hasara sawa na uchungu, afueni sawa ya kupata usalama na uoga wa mustakabali usio na uhakika, unaopatikana na kila mtu anayekimbia, ambao pia  kwa usawa wanastahili huruma yetu na msaada wetu." 

Bwana Grandi ameongeza, "tunaweza na lazima kukumbatia mshikamano, huku pia tukilaani kwa uthabiti vitendo vya ubaguzi na upendeleo".

Amesema ni muhimu "kukaa katika hali ya kutambua kwamba wakati shirika letu lipo kwa ajili ya kulinda haki za binadamu za watu waliolazimika kukimbia, baadhi yetu wamepitia matendo ya  kutengwa na ukosefu wa usawa."

Ukosefu wa usawa 

"Lazima tujaribu kupatanisha mkanganyiko huu wa ndani kwani tunashuhudia pia kukosekana kwa usawa duniani kote. Vita vya Ukraine na mzozo mbaya wa kibinadamu pia vinaleta changamoto na fursa za kuendelea kujitolea kwa bidii katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na ubaguzi."

Bw. Grandi amerejelea kauli yake kwamba raia wengi kutoka nchi jirani kama vile Poland, Hungary, Moldova, Slovakia na Romania wameonyesha "vitendo vingi vya ukarimu wa kukaribisha na huruma", kufungua mioyo na nyumba zao, kwa watu wa Ukraine. 

"Wimbi la kimataifa la msaada limetukumbusha ubinadamu wetu wa pamoja na nguvu ya mshikamano. Na wakati mimi na wafanyakazi wenzangu katika UNHCR tunaona kila siku jinsi jamii zinazowahifadhi na familia duniani kote zinavyonesha mshikamano,” amesema, "tunahitaji kuhakikisha kwamba ugawanaji wa uwajibikaji wa kimataifa unaimarishwa kwa wakimbizi wote, bila kujali wanatoka wapi." 

Kupambana na ubaguzi wa rangi 

Kamishna Mkuu huyo ameongeza kuwa kupinga ubaguzi wa rangi kunamaanisha "kutambua kikamilifu na kupinga ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa rangi. Leo na kila siku natoa wito kwa sisi sote kupaza sauti zetu dhidi ya sera, mazoea na tabia ambazo zinawatenga watu." 

Katika ujumbe wake kwa siku ya kimataifa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, amesema "kutambua maono ya ulimwengu usio na ubaguzi wa rangi unahitaji hatua kila siku, katika kila ngazi, katika kila jamii." 

Ametoa wito kwa watu wote kuungana na "ubinadamu wetu wa kawaida na kuzungumza kwa sauti moja kwa jili ya usawa, haki na utu kwa wote."