Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Mteja ananunua jibini kwenye duka la chakula katika soko la Esquilino huko Roma.

Hakuna anayependa lebo isipokuwa linapokuja suala la chakula:FAO

FAO/Alessia Pierdomenico
Mteja ananunua jibini kwenye duka la chakula katika soko la Esquilino huko Roma.

Hakuna anayependa lebo isipokuwa linapokuja suala la chakula:FAO

Afya

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO linasema biashara ya kimataifa inafanya kuwa vigumu zaidi kwa watu kufahamu ni nani anayezalisha chakula chakula tunachokula na anazalishaia wapi lakini Lebo za biashara zinazoaminika zinaweza kutusaidia kuziba pengo hili. 

Umefanya uamuzi wako kuwa na afya njema. Unakwenda kwneye bohari kutafuta moja kati ya bidhaa mbili, ukitafuta kilicho bora zaidi. Lakini ni kipi? Je, unachaguaje? Bila shaka unahitaji lebo!

FAO inasema lebo ni vitu ambavyo tunavichukua kama vya kawaida lakini ni muhimu sana katika afya na ubora wa maisha yetu.  

Lebo kwneye vyakula ni hakikisho kwamba chakula hiki ni kile tunachofikiria, ni sahihi na ni bidhaa gani vyenye virutubisho kama tunavyodhani.  

Lebo hutufunza kuhusu virutubisho na vyakula au madini yaliochanganywa kwenye vyakula hivyo. 
Huku biashra ya kimataifa ikiendelea kukua, ni vigumu ziadi kufahamu ni nani anayezalisha chakula na hata kufahamu ni wapi vyakula hivyo vinakotoka. 

Lebo zinazoaminika zinaweza kusaidia kuziba pengo hili.  

FAO na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO wanashirikiana kupitia tume ya Codex Alimentarius  kuweaka mfumo wa kimataifa wa lebo kwnye vyakula.  

Mashirika hayo yanasisitiza kwamba ni lazima mataifa yazingatie mfumo unaofaa wakati wa kuweka lebo kuhusan kwenye vyakula, hasa vile wanavyotaka kuuza kwneye soko la kimataifa. 

Makopo yaliyowekwa dungusi kakati inayozalishwa Tigray, Ethiopia, yakiwa kwenye duka la vyakula nchini Italia. Kulingana na utafiti unaoungwa mkono na FAO, vyakula vilivyowekwa alama ya Kijiografia (GI) vinaweza kukuza kipato cha wakulima
FAO/Alessia Pierdomenico
Makopo yaliyowekwa dungusi kakati inayozalishwa Tigray, Ethiopia, yakiwa kwenye duka la vyakula nchini Italia. Kulingana na utafiti unaoungwa mkono na FAO, vyakula vilivyowekwa alama ya Kijiografia (GI) vinaweza kukuza kipato cha wakulima

Haya ni mambo 6 muhimu kuhusu lebo za vyakula.

1.Salia na afya njema:

Lebo inakusaidia kufahamu vitu vilivyotumiwa kutengeneza vyakula hivyo unavyokula iwe ni vitamin, madini, mafuta nk.  
Habairi hizi ni muhimu kuhakikisha kwamba unakula vyakula vinavyokufaa. Kwa kutambua lebo unaweza kufuatilia aina ya virutubisho unavyokula ili kuepuka mapengo, hasa madini ya kawaida ya chuma na vitamini D. Unaweza kufuatilia uzito wako kwa manufaa ya chakula na mafuta yanayoingia mwilini, pia unaweza kupunguza kula sukari na chumvi na kuhakikisha kwamba unakula mlo sahili na sitahiki. 
Hivi vyote vinaweza kukusaidia kuepuka magonjwa, kama kisukari na aina mbalimbali ya magonjwa ya moyo.

2. Linda afya yako:

Kila mwaka watu zaidi ya milioni 600 huugua na wengine 420 000 wakifariki dunia kutokana na kula vyakula vyenye bakteria, vurusi, vimelea, vyenye sumu na kemikali.

Lebo hutoa onyo na habari muhimu kuhusu matumizi ya bidhaa kwa mfano, uhifadhi na maelekezo ya mapishi, pia vilivyomuhimu kuhakikisha chakula kipo salama. 

Mnunuzi akichagua matunda kwenye soko la Barcelona, ​​Uhispania. Picha: FAO/Alessia Pierdomenico
FAO/Alessia Pierdomenico
Mnunuzi akichagua matunda kwenye soko la Barcelona, ​​Uhispania. Picha: FAO/Alessia Pierdomenico
3. Inakusiadia kuepuka kununua bidhaa bandia :

Kuzuia utapeli ni moja wapo ya malengo makubwa kuhusiana na lebo za chakula.  
Bila kuwepo kwa lebo zilizothibitishwa kimataifa, wauzaji wa chakula wangeweza kutowatendea haki wateja wao kupitia utoaji wa habari za uongo wanapofungasha bidhaa zao.  
Unaponunua chokoleti, unataka kuhakikisha kwamba ni chokoleti yenyewe au hata kama ni samaki ni ile samaki unayotaka. 

4. Virutuimisho vya moja kwa moja vyenye madhara :

Asilimia 10 hadi 25 ya watu hupata madhara kutokana na aina fulani za vyakula katika nchi zilizoendelea.  
Vyakula vyenye mzio au allergy zaidi ni pamoja na karanga, soya, maziwa, mayayi, samaki, ngano na karanga za miti.

Ikiwa haukujua vilivyomo kwenye bidhaa ungeweza kula vinavyoweza kusababisha mzio, huku baadhi yao ikiwa ni mzio sugu. 

Lebo za vyakula hukusiadia kujua kile ambacho unapaswa kiujiepusha nacho . 

5. Hukuzuia kuharibu chakula:

Lebo za chakula zikisomwa kwa usahihi zinakusaidia usitupe chakula unachohofia.  
Siku chakula kilipotengenezwa na siku ya mwisho ya matumizi hukusaidia kufahamu bidhaa hiyo itakuwa salama kuliwa kwa kipindi gani.  

Inakusaidia kuepuka magonjwa kutokana na kula chakula kilichopitwa na wakati. Hata hivyo, kuchanganya maneno “bora kabla” na “tumia hadi” tarehe zinaweza kusababisha uharibifu wa chakula zaidi.  

Barani Ulaya, karibu 10% ya chakula kinachoharibiwa kinahusishwa na tarehe. Kufelimisha watumiaji na wanunuzi wote unaweza kusaidia kuzuia uharibifu wa chakula na kuhakikisha tarehe sahisi kwa sababu yakuhakikisha chakula kipo salama kwa mlaji. 

Mahindi yaliyopikwa kabla yanaonyeshwa kwa kuuzwa katika duka la mboga katika soko la Esquilino huko Roma, Italia.(16 Mei 2017).
©FAO/Alessia Pierdomenico
Mahindi yaliyopikwa kabla yanaonyeshwa kwa kuuzwa katika duka la mboga katika soko la Esquilino huko Roma, Italia.(16 Mei 2017).
6. Kuunga mkono chakula cha kienyeji au kinachozalishwa na wenyeji:

Lebo fulani ambazo huonesha asili ya chakula, kwa mfano kahawa ya Colombia yani Columbian Coffee (Colombia), Jibini ya Manchego (Spain), chai ya Darjeeling (India) au kahawa ya Kona (USA), vinaweza kuvutia wateja na kuongeza thamani kwa bidhaa kwa wazalishaji. 

Walaji hupenda kutambua bidhaa za kienyeji katika sehemu fulani na sifa zake kwa mfano ladha na ubora kuhusiana na sehemu fulani bidhaa zinapozalishwa. Katika utafiti uliofanywa na EBRD kwa ushirikiano na FAO, bidhaa za kiasili 9 zilioneshwa lebo hizo zilisaidia bei ya bidhaa hizo kuongezeka kwa silimia 20 hadi 50, leo wateja wake wameongezeka wakihusishwa na makaazi yao ya kijiografia, ubora na utamaduni. 

Lebo za chakula ni rahisi kupuuza unapokwenda kununua bidhaa unayotaka. 

Lakini ni muhimu kufahamu kwamba habari ni nguvu na pia nguvu hizi zinaweza kukusaidia kulinda afya yako. 

Huenda usipende kuitwa “mwenye msimamo mkali kuhusu afya” au “mtu anayependa sana chakula cha viwandani”, lakini unataka nyanya zako ziitwe nyanya na karanga zako kuitwa karanga! Tunatafuta dunia yenye chakula kwa wote wakiwa na uhakika kwamba chakula hicho ni salama. 
Huu ni msingi wa kujenga dunia huru bila njaa.