Chuki dhidi ya watu wenye asili ya Asia haistahili lazima ikomeshwe: UN

14 Septemba 2021

Ongezeko la chuki na uhalifu dhidi ya watu wenye asili ya Asia na visiwa vya Pasifiki nchini Marekani tangu kuzuka kwa janga la corona au COVID-19 limemhamasisha mmoja wa wasanii wa uchoraji hapa Marekani kuchora Sanaa mbalimbali zilizogonga vichwa vya Habari kote duniani 

Mfululizo wa kazi ya Sanaa ya Amanda Phingbodhipakkiya “I still Believe in this City” akimaanisha bado ana Imani na mji huu ilioneshwa mjini New York wakati machafuko ya chuki dhidi ya watu wa asili ya Asia yaliposhika kazi. 
Alipozungumza na UN News Bi. Phingbodhipakkiya anaeleza jinsi gani Sanaa inaweza kusaidia kusongesha haki za binadamu na kutibu vidonda. 
 

Bado Ninaamini katika Jiji Hili
MK Luff
Bado Ninaamini katika Jiji Hili

 Mnepo na matumaini wakati wakati wa kupinga chuki dhidi ya watu wa Asia 

Kuongezeka kwa uhalifu wa chuki dhidi ya watu wa asili ya Asia na Pasifiki nchini Marekani tangu mwanzo wa janga la COVID-19, kumemuhamasisha msanii Amanda Phingbodhipakkiya kutoa kazi za sanaa zenye zinazohusu watu wenye asili ya Asia.  
Kazi zake zimeonyeshwa katika maeneo mbalimbali ya umma karibu na Jiji la New York, na picha na ujumbe zilioubeba, vimekuwa vichwa vya habari duniani kote. 

Mabango yenye rangi za kung'aa, michoro na maonyesho yalionekana kwenye vituo vya mabasi, katika vituo vya treni za chini ya ardhi maarufu Marekani kama Subway na kwenye majengo ya kihistoria katika mji wa New York wakati wa majira chipukizi 2021, ikiwa ni sehemu ya mradi uliotumwa na tume ya Haki za Binadamu ya ujulikanao kama "Bado ninaamini katika jiji hili", akishiriki Bi Phingbodhipakkiya, kama msanii mkazi. 

 Wanatuinua kama walezi 

Bi Phingbodhipakkiya, mwanasayansi mtaalam wa masuala ya mishipa wa Marekani aliyegekia kuwa msanii ambaye alizaliwa Atlanta kwa wazazi wahamiaji kutoka Thailand na Indonesia, kwa muda mrefu amekuwa na sifa kubwa katika ulimwengu wa sanaa, na unaharakati wake wa kupigania masuala ya wanawake, sayansi, na jamii mara nyingi umekwenda zaidi ya majumbani na kwenye vyombo vya habari, umekwenda hadi kwenye maandamano na mikutano ya hadhara, na pia kwenye majengo na mabango ya kwenye barabara kuu. 

Bado nina amini kwenye jiji letu
MK Luff
Bado nina amini kwenye jiji letu

 
Lakini hatua yake ya kisanii kuhusu kuongezeka kwa chuki dhidi ya watu wenye asili ya Asia tangu kuzuka kwa janga la COVID-19 zimemletea hadhira kubwa hasa mfululizo wa : "Bado Ninaamini katika Jiji Hili" ambao umechapishwa katika vyombo vingi vya habari, pamoja na Jarida maarufu la Time, linaloonyesha mwamko mpya wa hasira na vurugu zinazoelekezwa kwa Wamerika wenye asili ya Asia 

Wakati kazi, ambazo zina picha za watu wenye asili ya Asia na  visiwa vya Pasifiki, zinakwenda sanjari na mtazamo wa sasa, maandishi yanayoambatana nazo humpa mtazamaji mtazamo tofauti, ulio na taarifa za juu ya hali mbaya iliyochagiza Sanaa hizo kama vile "Hapa ni nyumbani kwetu pia”, “mimi sio mlengwa wako” “Mimi sikukusababishia kuumwa” kaul inayowalenga watu wenye asili ya Asia bila Ushahidi wowote kwamba wao ndio chanzo cha kusambaza COVID-19. 

Bi Phingbodhipakkiya anasema kwamba takwimu zilizoonyeshwa kwenye mabango na michoro zinawakilisha "watetezi wenye ujasiri, wenye matumaini, kutokana na mashambulizi haya mabaya dhidi ya jamii yetu. Wanatuinua kama walezi, wakitulinda, na wakituhimiza kutetea haki zetu ”. 
 

Bado naamini kwenye jiji la New York: Mchoro wa msanii unaopinga ubaguzi kwa watu wa Asia
UN Video
Bado naamini kwenye jiji la New York: Mchoro wa msanii unaopinga ubaguzi kwa watu wa Asia

 Sanaa na haki za binadamu 

Maonyesho ya sanaa ya umma yamesifiwa na mwenzake mtetezi wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Derrick León Washington, mtaalam wa kitamaduni wa anayeishi  New York, Marekani, mcheza densi na mtunzi, ambaye anaamini kuwa sanaa ni muhimu katika kukuza haki za binadamu: "sanaa kama ya Amanda ni njia muhimu ya kuanza mazungumzo magumu. Imeunganishwa na uzoefu wa kuishi, na inatusaidia kuzifikia na kugusa jamii tofauti. " 

Kazi za sanaa, anasema Bwana Washington, "huzungumza na ujasiri wa Wamarekani wenye asili ya Asia wakati wanakabiliwa na vurugu za chuki dhidi ya Waasia. Lakini, hii sio hadithi tu ya New York au Marekani, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea "wasiwasi mkubwa juu ya kuongezeka kwa mashambulio kama hayo ulimwenguni. " 

"Ubaguzi wa rangi dhidi ya Waasia na Wakazi wa Visiwa vya Pasifiki sio jambo geni", anasema Carmelyn Malalis, mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu ya New York. "Sote tuna hadithi kutoka kwa vijana wetu, lakini ni kweli kwamba mwaka jana ulikuwa mbaya sana, kwa sababu ya janga hilo la COVID-19." 

Bi Malalis anasema kwamba viwango vya kuongezeka kwa chuki dhidi ya watu wenye asili ya Asia vilifanyika katika muktada wa kuongezeka kwa aina zote za ubaguzi wa rangi, huko New York na kwingineko. "Katika mwaka uliopita harakati za kutanabaisha Maisha ya Weusi ni muhimu zimekuwa zikipambana dhidi ya wanaowachukia watu weusi, na sasa wanaowapinga watu wa asili ya Asia, chuki dhidi ya Wayahudi na aina zingine za chuki dhidi ya wageni. Huu ni mji wenye tofauti nyingi, na tunataka kuona mshikamano kati ya jamii zetu zote tofauti.” 
 

Bado naamini kwenye jiji letu
MK Luff
Bado naamini kwenye jiji letu

 Naomba tutambue nguvu zetu wenyewe 

Wakati huo huo kazi za sanaa za "Ninaendelea Kuamini Jiji Hili" zilikuwa zinaoneshwa katika jiji la New York, Bi Phingbodhipakkiya alizindua kipande kingine, cha kusikitisha zaidi, pia kwa kushirikiana na Tume ya New York ya Haki za Binadamu, Sanaa aliyoiita "Naomba tutambue nguvu yetu mwenyewe ”. Ilikua majibu yake kwa kupigwa risasi kwa watu wengi mnamo Machi 2021, tukio lililosababisha vifo vya watu wanane, sita kati yao walikuwa wanawake wenye asili ya Kiasia. 

"Sanaa hizi zimekuwa polepole kutoka kwa hadithi za pamoja za unyanyasaji dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Asia na Visiwa vya Pacific (AAPI), lakini ilikuwa bayana kwa kila mtu anayepitia jambo gumu; ilikuwa nafasi kwao kutua mzigo wao chini ”. 

Waathirika na manusura wa mashambulio na aina zingine za unyanyasaji walichapisha hadithi zao bila kujulikana, mara nyingi kwa kibinafsi na za kutisha, kwa fomu maalum mtandaoni.  

Kila ulistahili kuchapishwa na uiliwasilisha hadithi hizo kwenye ribboni za karatasi, wakati ukiwasha taa ya giza lililopo. Bi Phingbodhipakkiya kisha akageuza hadithi hizo kuwa sanaa ngumu za kutundika. 

Msanii anasema kwamba anatumai maonyesho hayo ya Sanaa yatasaidia kubadili maumivu na machungu ya kila hadithi kuwa "njia mpya ya amani na upole, na njia mpya ya kusonga mbele.” 

"Mara nyingi", anaongeza "tunapoona vitendo vibaya, tunageuka upande mwingine. Lakini, kwa kufunga mlango kwa wengine, tunafunga mlango kwa ubinadamu wetu wenyewe. Sanaa inaweza kuurudisha. ” 

NOTE: Makala hii ni moja wapo ya mfululizo wa makala zinazohusiana na maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka ishirini ya Azimio la Durban la Umoja wa Mataifa linalochukuliwa kuwa hatua muhimu katika vita vya ulimwengu dhidi ya ubaguzi wa rangi. 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter