Ni muhimu kuwe na mabadiliko ili bara Afrika lifurahie maendeleo ya kiteknolojia-Bi.Mohammed

5 Septemba 2019

Tuko katika hali ya kuingia nyakati mpya kufuatia mabadiliko ya kiteknolojia, wakati ambapo maendeleo ya kiteknolojia yanaleta ahadi nyingi lakini pia mambo mengi yasiyotabirika.

Hivyo ndivyo ilivyoanza hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed kwenye kongamano la dunia kuhusu uchumi Afrika, WEF huko Afrika Kusini hii leo.

Bi. Mohammed amesema hali hiyo inaongeza changamoto nyingine katika maswala ambayo tayari jamii zinaendelea kukabiliana nazo ikiwemo ukatili dhidi ya wanawake na wasichana na vijana kwani mitandao ya kijamii inatumika kulenga kutishia na kubinya sauti za wanawake na inatumika kuchangia ukatili katika mifumo mbali mbali.

Amesema ili kukabiliana na hali ya sintofahamu na athari zake kwa ushitikiano ni muhimu huku akitoa shukrani kwa jukwaa la uchumu duniani kwa ajili ya msaada wao huku ushirikiano ukiendelea kuimarika na kuchukua sura tofauti na kuweka mazingira mapya kwa ushirkiano jumuishi na wenye haki.

Naibu Katibu Mkuu huyo amesema teknolojia mpya zimeenea kwa kasi kubwa kuliko uwezo wa kuelewa au kusimamia athari zake kuhusu maendelea, amani na usalama na haki za binadamu.

Ameongeza kwamba changamoto ya pamoja ni kuleta pamoja serikali, mashirika ya kiraia na jamii ya wasomi na viwanda vyenyewe ili kuimarisha mazuri yatokanayo na teknolojia na kusimamia kwa njia bora zaidi madhara yanayoweza kutokea kuathiri amani, usalma na kukandamiza kufurahia kwa haki za binadamu.

Bi. Mohammed amesema maendeleo katika teknolojia yanatoa matumaini katika kuongeza kasi kufikia malengo ya maendeleo endelevu, “teknolojia ya kidjitali inawaleta watu pamoja kote ulimwenguni na kuwawezesha kupata tarifa na huduma katika gharama ya chini. Ameongeza kwamba, “katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, mamilioni ya watu katika nchi zinazoendelea walifungua akaunti za fedha kufuatia uwepo wa vitambulizho vya vitambulisho na teknolojia za simu za mkononi.

Hata hivyo Bi. Mohammed amesema licha ya hatua zilizopigwa lakini watu wanaoishi katika umasikini hawanufaiki na teknolojia kikamilifu, “dunia ina muundo mpya wa ukosefu wa usawa; waliowezeshwa kwa maswala ya kidijitali kwa upande mmoja na wale wamekosa maendeleo hayo kwa upande mwingine.” Huku wanawake ni idadi kubwa ya waliokosa maendeleo hayo.

Bi. Mohammed amesema kuna baadhi ya mifano ya matumizi bora ya kiteknolojia barani Afrika ambayo inatoa matumaini ikiwemo, “Rwanda ambako dawa zinawasilishwa kwa kutumia ndege zisizo na rubani, Uganda ambako koti janja lina uwezo wa kupima joto la mwili, na mapigo ya moyo na hali ya mapafu inasaidia madakatari kugundua ugonjwa wa vichomi, nchini Nigeria ambako ukusanyaji wa taarifa kutoka kwa jamii kunatoa msaada wa kifedha kwa maelfu ya wakulima, Kenya ambako apu inatumika kusajili ardhi na Afrika Kusini ambako picha kwa njia ya ndege zisizo na rubani zinatumika kutafiti matatizo ya mazao ya mimea katika msimu ya ukame.”

Bi Mohammed amesema ili kufikia faida kamili za mabadiliko ya nne ya viwanda, sera za kitaifa, sheria na usimamizi zinapaswa kutoa muongozo bora na kuweka mazingira kwa ajili ya maendeleo ya kiteknolojia.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud