Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi uliofadhiliwa na IFAD nchini Brazil wakisaidia kijiji kilichohisi kimetengwa na dunia

Wakulima wa vijijini
World Bank/Scott Wallace
Wakulima wa vijijini

Mradi uliofadhiliwa na IFAD nchini Brazil wakisaidia kijiji kilichohisi kimetengwa na dunia

Ukuaji wa Kiuchumi

Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD umefanikiwa kubadili maisha ya wananachi waliohisi wametengwa na dunia huko Bahia nchini Brazil ambao hata miundombinu ya kuwafikia ilikuwa shida lakini sasa wanauza bidhaa zao kwa njia ya mtandao. 

Brejo Dois Irmãos,ni kijiji kidogo kilichoko katika jimbo la Bahia kaskazini -Mashariki mwa Brazil, ilikufika katika Kijiji hicho inabidi kupita kwenye barabara ya mchanga yenye urefu wa kilometa 12 ambayo magari mengi hayawezi kufika huko.

Jumla ya familia 200 zinazoishi Brejo zinaona kama zimetengwa na dunia kama anavyoeleza aliyekuwa rais wa jumiya hiyo Cosme Aves de Sousa “Changamoto kubwa ya kuishi Brejo nikwamba kuifikia jamii hii ni ngumu sana”

Jamii hii imejificha na hazina ya thamani kubwa ya BURITI, mti wa mtenda ambao kwa lugha ya kwao ukimaanisha “Mti wa Uzima”. Mti huu ambao kila kitu chake kuanzia matawi mpaka matunda yana thamani kubwa kwakuwa na uwezo wa kutoa juisi,dawa na bidhaa mbalimbali lakini umekuwa na thamani ndogo kiuchumi kwakuwa imekuwa ngumu kutengeza bidhaa na kuuza.

Hata hiyo hali hiyo imebadilika baada ya Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD kufika katika kijiji hicho na kufadhili mradi ambao mbali na kuwapatia mafunzo pia uliwapatia vifaa vya kisasa.

“Mradi wa Pro-Semiarid umetufungulia milango, umetufundisha mbinu mbalimbali za mauzo, tumuuzie nani na kuongeze vipi dhamani kwenye bidhaa zetu” amesema Cosme Aves de Sousa

Kwakutumia mashine mpya, wanakijiji sasa wanaweka tunda la mtende kwenye mashine ambayo inaosha, kumenya na kusaga na kupata malighafi ambayo inatumika kwenye bidhaa za chakula na urembo, kazi hii iliyokuwa unachukua siku kadhaa sasa inafanyika kwa saa kadhaa.

Rais wa sasa wa chama cha jamii hiyo Eliane Ribeiro anasema “Usindikaji ilikuwa kazi ngumu, iliyotumia nguvu kazi kubwa na ngumu. Tulikuwa siku nzima tunakaa chini kwasababu hatukuwa na miundombinu ya kutufanya tusimame. Tulikuwa tunatoa maganda ya tunda moja baada ya jingine na kisha kwenda kuyaanika nje kwenye jua ili yakauke, kisha tunayaleta ndani tunayaosha na kwenda kuyaanika tena nje yakauke. Lakini sasa hii yote ni kazi moja tunayaweka kwenye mashine tuu na kazi yote inafanyika na kumalizika. Haya ni maendeleo makubwa sana kwetu.”

Kupitia mradi huu wanakijiji wameanzisha kiwanda kinachochakata zaidi ya tani 40 za matunda ya mtende kwa mwaka.

Upatikanaji wa mtandao wa intaneti ilikuwa vigumu sana hapo awali. Lakini mradi huu uliwezesha kuwaunganisha na mitandao ya kijamii na sasa wanauza bidhaa zao mtandaoni na kipato cha wananchi kimeongezeka kwa asilimia 30 mpaka 40. Mafanikio mengine yaliyopatikana ni wanawake kujumuisha katika vikao vya kufanya maamuzi na kuleta maendeleo na sasa wananchi hawa hawaoni tena kama wametengwa na dunia.