Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada ya kibinadamu na maendeleo vinapaswa kwenda pamoja-UN

Mkuu wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Achim Steiner (kulia) na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Mark Lowcock (kushoto) wakiwa na wataalamu wa lishe mjini N’Djamena.
@OCHA/Eve Sabbagh
Mkuu wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Achim Steiner (kulia) na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Mark Lowcock (kushoto) wakiwa na wataalamu wa lishe mjini N’Djamena.

Misaada ya kibinadamu na maendeleo vinapaswa kwenda pamoja-UN

Msaada wa Kibinadamu

Mkuu wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Achim Steiner na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Mark Lowcock, hii leo Oktoba 7 wameikamilisha ziara yao ya kwanza ya pamoja nchini Chad.

Wakiwa mjini N’Djamena, viongozi hao wametaka ushirikiano katika kutoa misaada na masuala ya maendeleo katika nchi hiyo iliyoko afrika ya kati wakati wa kupabana na umaskini, ukosefu wa makazi, utapiamlo na ukosefu wa huduma za msingi za kijamii.

Lowcock na Steiner wametembelea kituo cha lishe cha hospital ya ushirikiano kati ya Chad na China katika mji mkuu N’Djamena ambako zaidi ya watoto elfu 16 wenye utapiamlo wanalazwa kila mwaka. Mwaka huu matatizo ya utapiamlo mkali yaliongezeka kufikia asilimia 57 katika kituo hicho kinachoeneshwa na wizara ya afya kwa msaada wa washirika wa kimataifa.

"Nimeguswa sana na shida ya wanawake  na watoto niliyoikutana katika kituo cha lishe N'Djamena leo, ninapongeza jitihada na matendo yaliyofanyika ili kukabiliana na moja ya tatizo la kubwa la lishe ambalo watu wa Chad wamekabiliwa nalo. Lakini kwa kuanzia, changamoto kubwa ni kuzuia Watoto kuwa katika hali hii. Misaada ya kibinadamu inaweza kuokoa maisha, lakini suluhisho ni maendeleo, maendeleo ya kiuchumi na maisha bora. Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia Serikali, tunatakiwa kuongoza katika mchakato huu” Lowcock amesema.

Pia viongozi hawa wawili wa Umoja wa Mataifa wamekutana na viongozi wa serikali na wabunge, na kujadili mipango ya maendeleo ya taifa, kupunguza umaskini, hali ya kikanda, na mkutano wa hivi karibuni mjini Berlin kuhusu mgogoro wa ziwa Chad. Lowcock na Steiner wametaka kuwepo kwa serikali na uongozi madhubuti na ahadi za muda mrefu kutoka kwa wadau wote, ikiwa ni pamoja na wafadhili, kuunga mkono mahitaji ya dharura ya kaya zilizoathirika na upatikanaji wa huduma za msingi za kijamii kwa wote.

Ziara hii inahitimisha safari ya siku tatu nchini Nigeria na Chad, wakati maafisa wawili wa Umoja wa Mataifa wakiangalia njia ambazo watoa misaada ya kibinadamu na maendeleo wanaweza kuunga mkono jitihada za kitaifa za msaada, ikiwa ni pamoja na mgogoro wa Bonde la Chad Bonde.

Huko Nigeria, Steiner na Lowcock walisisitiza zaidi msaada wa kupunguza mgogoro wa kibinadamu na kujenga upya maisha katika eneo lililoharibiwa na mgogoro kaskazini-mashariki mwa nchi.