UN imeazimia kutokomeza kabisa silaha za nyuklia-Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekaribisha maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kupitishwa kwa mkataba wa kimataifa wa kuzuia silaha za nyuklia, TPNW.
Amesema kupitishwa kwa mkataba huo, Julai 7 mwaka 2017 na mataifa 122, kunadhihirisha uungwaji mkono wa jamii ya kimataifa kuhusu suala liliopo la kukomesha tishio la silaha za nyuklia.
Ameongeza kuwa hadi sasa mataifa 59 ndio yametia sahihi mkataba huo wa TPNW na mengine 11 yakiwa yameuratibu na endapo mataifa 50 yatauratibu hapo ndipo utaanza kutekelezwa rasmi, na kuwa chombo muhimu katika kutokomeza silaha hizo.
Katibu Mkuu ,kupitia taarifa iliyotolewa leo mjini New York Marekani na naibu msemaji wake Farhan Haq, amesema kuwa Umoja wa Mataifa, umeazimia kuondoa kabisa silaha za nyuklia kama será yake ya juu ya unyanganyaji wa silaha hizo.