Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola 13 bilioni zilichangishwa kusaidia binadamu mwaka 2017

Uchotaji maji katika daraja lililobolewa kwa mashambulizi Yemen. OCHA linasaidia watu walio katika hali kama hiyo 2017
Picha ya OCHA/Giles Clarke
Uchotaji maji katika daraja lililobolewa kwa mashambulizi Yemen. OCHA linasaidia watu walio katika hali kama hiyo 2017

Dola 13 bilioni zilichangishwa kusaidia binadamu mwaka 2017

Masuala ya UM

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA ilifanikiwa kutoa huduma mbalimbali za kibinadamu kwa watu milioni141mwa 2017.

Hayo yamo katika ripoti ya OCHA ya kila mwaka iliyozinduliwa leo.

Ripoti hiyo inamulika mwaka 2017 ambao inasema, mahitaji ya misaada ya kibinadamu yalifikia kiwango cha juu.

 Idadi ya watu waliohitaji msaada ilikuwa kubwa kutokana na migogoro katika sehemu tofauti za dunia kama vile machafuko ya kisiasa, mabadilikoya tabianchi na pia matokeo ya majanga ya asili.

Isitoshe, ripoti inaongeza kuwa OCHA, mwaka wa 2017, iliweza kutafuta ufadhili na kuboresha maisha ya watu waliojikuta katika njia panda za migogoro katika nchi kama Jamhuri ya Afrika ya Kati, maeneo ya bonde la ziwa Chad, Syria na Yemen.Kwa mujibu wa ripoti hiyo, OCHA iliepusha njaa iliyotishia watu milioni 20 kaskazini-mashariki mwa Nigeria, Somalia, Sudan Kusini na Yemen.