Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Saudia tendeeni haki watetezi wa haki mnaowashikilia-OCHA

. Picha: UM/Loey Felipe
Bendera ya Saudi Arabia (kati).

Saudia tendeeni haki watetezi wa haki mnaowashikilia-OCHA

Haki za binadamu

Watetezi wa haki za binadamu wamekamatwa nchini Saudi Arabia jambo ambalo limekosolewa na  ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa-OHCHR na kuitaka serikali ya nchi hiyo kueleza wamewekwa wapi na watetendewe haki.

Msemaji wa ofisi hiyo Elizabeth Throssell ametoa msimamo wao hii leo huko Geneva, Uswisi alipozungumza na waandishi wa habari.

 (Sauti ya Liz Throssel)

 “ Tangu Mei 15, yaonekana kuwa takriban wanaharakati 13 wengi wao wanawake, wamekamatwa, ingawa wannne  kati yao yaripotiwa wameachiliwa huru.”

Msemaji wa OHCHR amekielezea kitendo hicho kama cha kukanganya  kufuatia kile kilichoitwa kulegeza msimamo katika taifa hilo la uarabuni ambalo kuna mageuzi fulani yanayosemekana kufanywa na mrithi wa ufalme, Mohammed bin Salman.

Baadhi ya mageuzi ni kuondoa marufuku kwa wanawake kuendesha magari, mipango ya kufungua majumba ya sinema na pia mageuzi mengine ya kijamii na kiuchumi.

 Akinukuu vyombo vya habari vya Saudia, Bi. Throssell amesema,

(Sauti ya Liz Throssel)

“Madai dhidi ya waliobaki ndani, wanawake sita na wanaume watatu, yaonekana ni makubwa na yanaweza kusababisha hukumu kali”.

Ameomba mamlaka za Saudia Arabia zitoe taarifa kuhusu mahabusu hao pamoja na mwanamke mmoja ambaye inadaiwa kuwa hana mawasiliano yoyote yale.