Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Monsoon kuwaweka roho juu wakimbizi wa Rohingya:UNHCR

Warohingya watumia vyelezo kukimbia Myanmar. © UNHCR/Andrew McConnell

Monsoon kuwaweka roho juu wakimbizi wa Rohingya:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limeonya kwamba msimu wa pepo kali na mvua za monsoon utawaweka hatarini maelfu ya wakimbizi wa Rohingya walioko Bangladesh na hivyo likishirikiana na wadau wengine wanajiandaa kukabiliana na athari zake.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi , msemaji wa UNHCR Andrej Mahecic amesema msimu huo wa monsoon unaojumuisha vimbunga unaweza kuwa na athari kubwa kwa maelfu ya wakimbizi wa Rohingya wanaoishi kwenye makambi yaliyofurika ya Cox Bazar.

Serikali ya Bangladesh imesema inalitambua hilo na inajiandaa kukabiliana nalo wakati mashirika ya kibinadamu na Umoja wa Mataifa wameandaa kundi maalumu la dharura wakati wa athari hizo ikiwemo maradhi ya kuambukiza, kusambaratishwa kwa malazi, vituo vya afya vya muda, vyoo , na visima kufurika au kusombwa na barabara kutopitika hali  ambayo itaathiri uingizaji wa misaada.

Ameongeza kuwa…

(SAUTI YA ANDREJ MAHECIC)

"Matokeo ya awali ya tathimini  ya hatari ya makazi hayo makubwa kabisa duniani ya wakimbizi ya Kutapalong na Balukhali yanayohifadhi zaidi ya wakimbizi 569,000 , yanaonyesha kwamba takribani wakimbizi 100,000 watakuwa katika hatari ya kifo kutokana na maporomoko ya udongo na mafuriko."