Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lacroix yuko CAR kusaka suluhu ya machafuko mapya

Lacroix yuko CAR kusaka suluhu ya machafuko mapya

Mkuu wa operesheni za amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix yuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ili kusaidia kupata suluhu ya kuzuia kuendelea kwa machafuko yanayotishia mchakato wa amani.

Katika ziara hiyo ya siku tatu inayomalizika leo Jumanne Lacoix amekutana na maafisa wa Umoja wa Mataifa nchini humo, viongozi wa serikali na wawakilishi wa asasi za kiraia mjini Bangui na kuwaambia..

(LACOIX CUT 1)

"Nimekuja kwa sababu tunahitaji kwa pamoja na uongozi wa serikali, asasi za kiraia na marafiki zetu kutoka MINUSCA kuangalia jinsi ya kuzuia suluhu ya hatari iliyopo leo , isitupokonye hatua kubwa tuliyopiga katika maika michache iliyopita."

Kuhusu wanaochochea machafuko amesema..

(LACOIX CUT 2)

“Nataka kusisitiza kwamba wale wanaohusika na hotuba za chuki, mgawanyiko, wale wanaotaka kuisambaratisha jamii kwa misingi ya kikabila au kidini watawajibishwa kwa vitendo vyao. Kuna mahakama ya kimataifa ya uhalifu, kuna mahakama maalumu ya uhalifu, kuna mfumo wa sheria wa CAR ambazo tunashirikiana nazo , na vitendo hivyo lazima vitaadhibiwa."