Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kisa cha pili cha Ebola chagunduliwa Sierra Leone

Kisa cha pili cha Ebola chagunduliwa Sierra Leone

Nchini Sierra Leone, mtu wa pili amegunduliwa kuwa kirusi cha homa ya Ebola. Ametangaza leo msemaji wa Shirika la Afya duniani WHO, Tarik Jasarevic.

Kisa hicho cha pili kinafuata kisa cha kwanza kilichogunduliwa nchini humo wiki iliyopita saa chache tu baada ya Sierra Leone kutangaza kuwa imetokomeza Ebola.

Bwana Jasarevic amesema mgonjwa huyo ambaye sasa hivi anatibiwa alikuwa ameanza kuugua akiwa kwenye karantini. Aliwekwa karantini kwa kuwa alikuwa shangazi ya mgonjwa wa kwanza na alikuwa anahumhudumia wakati wa ugonjwa wake.

Daktari Magda Robalo ni mkurugenzi wa magonjwa ya kuambukiza wa WHO katika kanda ya Afrika, mjini Brazzaville, Congo.

(Sauti ya Bi Robalo)

Licha ya kushuhudia Liberia, Sierra Leone na Guinea kuweza kusitisha mlipuko huo mkubwa, hatari haijaisha. Tunapaswa kuendelea kuwa makini, kuimarisha utayari wetu. Uwezo wetu wa kukabiliana na mlipuko wowote mpya unapaswa kuwa kipaumbele chetu.”