Mtaalam, aonya juu ya kufanya kuwa jinai huduna binafsi za dharura Uturuki:

9 Disemba 2013

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu haki ya afya Anand Grover, na jumuiya ya madaktari duniani  (WMA)  leo wamelitaka bunge la Uturuki (Meclis) kufikiria upya mswada ambao utafanya kuwa ni kosa la jinai kwa madaktari binafsi  waliofuzu kutoa thuduma wakati wa dharura baada ya kuwasili kwa gari la wagonjwa la serikali.

Mwakilishi huyo anasema endapo mswada huo utapitishwa na kuwa sheria utakuwa na athari kubwa hasa katika uwepo na upatikanaji wa huduma za afya za dharura katika nchi hiyo ambayo hukumbwa na majanga ya asili , na demokrasia ambayo haina kinga ya maandamano.

Amesema kupitishwa kwa sheria na sera zinazofanya kuwa jinai utoaji wa huduma za afya kwa watu wanaopinga serikalikamavime waandamanaji wa kisiasa, kutawafanya wahudumu wa afya kuogopa kutoa huduma wakihofia kushitakiwa.