Familia za wale waliotoweka kwa lazima na mashirika yasiyokuwa ya serikali wahitaji kulindwa: UM

29 Agosti 2013

Mashirika ya umma na watu wa familia ambazo wapendwa wao hupotea wanahitaji kulindwa kutokana na vitisho huku pia wakihitaji kusaidiwa katika kazi zao. Hii ni kwa mujibu wa wataalamu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kabla ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya waathiriwa wa vitendo vya kutoweka kwa lazima kwa watu siku ambayo itaadhimishwa kesho tarehe 30.

Familia za wale waliotoweka na mashirika yasiyokua ya kiseriklia mara nyingi ndio sauti nchini mwao wakitaka ukweli kubainika na sheria kuchukua mkondo wake kutaka kubaini ukweli kuhusu hatma za waliotoweka kwenye nyanja za kitaifa na kimataifa. Wataalamu hao wanasema kuwa wengi wanakabiliwa na chamngamoto za kudhulumiwa na kukabiliana na vizingiti wanapofanya jitihada za kukabiliana na suala la kutoweka kwa watu kwa lazima.

Ushuhuda kutoka kwa baadhi ya watu wanaofanaya jitihada za kutaka kujua kilichowapata wapendwa wao wanasema kuwa mara baada ya wao kuwasilisha kesi zao kwenye makundi husika maafisa wa polisi walianza kufika nyumani kwao wakiwaliza ni kwa nini wameishtaki serikali. Wataalamu hao sasa wanazitaka serikali kuchukua hatua za kulinda familia za watu waliotoweka na mashirika ya umma yanaohusika kwenye masuala ya kutoweka kwa lazima kwa watu na kuwakinga kutokana na dhuluma zozote zile.