Kipindi cha kati ya mwaka 2001 na 2010 kilirekodi viwango vya juu zaidi vya joto:WMO

3 Julai 2013

Ulimwengu ulishuhudia athari nyingi zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa kati ya mwaka 2001 – 2010 ambao ulikuwa ni mwongo wenye joto zaidi tangu kuanza kunakilikiwa kwa viwango vjoto mwaka 1850 kwa kujibu wa ripoti mpya kutoka kwa shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Ripoti hiyo ilichambua viwango vya joto kote dunia na sehemu kadha na hali zingine zikiwemo joto hasa barani Ulaya na Urusi, tufani Katrina nchini Marekani . tufani ya Nargis nchini Myanmar, kingazi kwenye bonde la Amazon, Australia pamoja na mafuriko nchini Pakistan. Mwongo kati ya mwaka 2001 na 2011 ulitajwa kuwa wenye viwango vya juu zaidi vya joto ardhini na baharini. Hali hii ilifuatwa na kuyeyuka kwa barafu kwenye eneo la Arctic , Geenland na eneo la Antarctic. Kutokana na kuyeyeyuka kwa barafu hizi viwango vya maji baharini vilipanda kwa karibu milimita tatu kila mwaka kinyume na vilivyorekodiwa awali vya milimita 1.6 kila mwaka. Ripoti ya WHO inaonyesha kuwa viwango vya joto vilipanda kwa hara kaunzia mwaka 1971 hadi mwaka 2010 huku vya juu zaidi vikishuhudiwa kati ya mwaka 1991-2000 na mwaka 2001 hadi mwaka 2010. Mkurugenzni mkuu wa shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO Michel Jarraud anasema kuwa utafiti zaidi unafanyika kwa sasa kubaini iwapo matukio yanayoshuhudiwa yana uhusiano na mabadiliko ya hali ya hewa au na mambo tu kiasili.