Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uingereza kujitahidi kumaliza sintofahamu ya wasio na utaifa:UNHCR taa za miale ya jua

Uingereza kujitahidi kumaliza sintofahamu ya wasio na utaifa:UNHCR taa za miale ya jua

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limekaribisha hatua za kujidhatiti za Uingereza ambazo zimeanza kutekelezwa April 6 kukabiliana na tatizo la wasio na utaifa. Joshua Mmali na maelezo zaidi

(SAUTI YA JOSHUA)

Hatua hizo zinawaruhusu watu wasio na utaifa ambao kwa sasa wanaishi Uingereza kwa kujitenga na kukabiliwa na hatihati za kisheria kufuata mfumo upasao ili watambuliwe rasmi kama ni watu wasio na utaifa na kuhalalishwa kisheria uwepo wao Uingereza.

UNHCR inasema hiyo ni hatua nzuri na muhimu sana na kusema mikakati hiyo mipya ni mfano wa kuigwa na mataifa mengine  ambayo yaliridhia mkataba wa mwaka 1954 unaohusiana na hali ya watu wasio na utaifa ambayo hadi sasa hayajatekeleza mkataba huo kwa kuanzisha hatua za kuwatambua rasmi na kuwalinda watu wasio na utaifa.

Kuanzishwa na kutekelezwa kwa hatua hizo nchini Uingereza ilikuwa ni moja ya mapendekezo yaliyoainishwa kwenye utafiti uliofanywa na UNHCR na shirika lisilo la kiserikali la Partner Asylum Aid mwaka 2011.

Utafiti huo ulibaini kwamba kuna watu takribani 150 hadi 200 ambao wanaomba hifadhi ya ukimbizi kila mwaka nchini Uingereza na wanaorodheshwa kama watu wasio na utaifa na idara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo.

Uingereza iliridhia mikataba yote wa mwaka 1954 wa watu wasio na utaifa na ule wa mwaka 1961 unaohusu upunguzaji wa watu wasio na uta