Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna maendeleo endelevu kama kuna njaa: FAO

Hakuna maendeleo endelevu kama kuna njaa: FAO

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO Graziano Da Silva anasema kuwa hakutakuwepo na maendeleo ya kudumu duniani ikiwa watu wataendela kuhangaishwa na njaa.

Akizungumza kwenye mkutano wa jumuia ya nchi za Amerika kusini, Carribean na Ulaya, Da Silva amesema kuwa mataifa sasa yana fursa ya kutoa mapendekezo kuhusu siku za usoni zilizo na usawa wa kijami na kiuchumi ambazo kila mmoja duniani anahitaji. Jason Nyakundi na taaarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)