Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitishwa na mwendelezo wa ghasia nchini Syria

Ban asikitishwa na mwendelezo wa ghasia nchini Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amesema anasikitishwa na mwendelezo wa ghasia nchini Syria katika siku za karibuni na hatari kubwa inayokabili raia kwenye maeneo ambako kuna mapigano.

Bwana Ban amekaririwa na msemaji wake akieleza masikitiko hayo huku akishutumu mashambulizi ya silaha kwenye maeneo ya raia ambapo amerejelea kauli yake ya kutaka pande zote katika mzozo nchini Syria kuacha mapigano. Jason Nyakundi na taarifa zaidi.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)