Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yashirikiana na serikali ya Ufilipino kufuatilia athari za kimbunga Bopha

IOM yashirikiana na serikali ya Ufilipino kufuatilia athari za kimbunga Bopha

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM linashirikiana na serikali ya Ufilipino na mashirika mengine ya misaada ya kibinadamu kutathmini athari za kimbunga Bopha wakati huu ambapo kinaendelea kupiga eneo la Mindanao kusini mwa nchi hiyo.

Kasi ya kimbunga hicho imepunguzwa kutoka Tano hadi Tatu na ripoti za awali zinaonyesha kuwepo na idadi ndogo ya waathirika.

Msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe akizungumza mjini Geneva, Uswisi amesema watu wapatao 155,000 walihamishiwa katika makazi 187 ya dharura huko Mindanao na kwamba watumishi 120 wa shirika hilo wako eneo hilo wakishirikiana na maafisa wa serikali na wale wa mashirika ya kimataifa na kitaifa kutathmini mahitaji ya wananchi.