Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yawarejesha kwao raia wa Filipino waliokwama Syria

IOM yawarejesha kwao raia wa Filipino waliokwama Syria

Kiasi cha raia 261 wa Ufilipino waliokuwa wamejikusanya kwenye ubalozi wa Filipini nchini Syria kwa ajili ya kupata hifadhi ya muda, wamerejea nchini mwao kwa kusafirishwa na ndege ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM.

Hii ni mara ya pili kwa ndege ya shirika hilo kuwarejesha raia wa Ufilipino na mara ya kwanza ilikuwa mwezi August.

Tangu kuzuka kwa hali ya sintofahamu nchini Syria mwaka uliopita 2011, shirika hili la Umoja wa Mataifa limewafadhilia zaidi ya raia 800 wa Ufilipino kurejea nyumbani.

Shirika hilo linafanya kazi kwa kushirikiana ubalozi wa Filipin mjini Damascus kuratibu hatua za kuwarejea nyumbani raia hao waliokuwa wakifanya kazi katika maeneo mbalimbali