Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mshindi wa hotuba ya Katibu Mkuu kutoka Kenya ataka vijana wawe na usemi zaidi

Mshindi wa hotuba ya Katibu Mkuu kutoka Kenya ataka vijana wawe na usemi zaidi

Wallace Chwala, mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi Kenya, ni mmoja wa washindi wa uandishi wa mfano wa hotuba ambayo ingetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, wakati wa kufungua kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Shindano hilo la uandishi wa hotuba ya Katibu Mkuu, liliandaliwa na Taasisi ya Brookins kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa, na ikawashirikisha vijana kutoka kote duniani. Washindi walialikwa mjini New York kukutana na Katibu Mkuu, Ban Ki-Moon kwenye Siku ya Kimataifa ya Amani.

Baadaye, Wallace alitembelea studio za Radio ya Umoja wa Mataifa na kuzungumza na Joshua Mmali kuhusu ushindi wake na mtazamo alio nao kuhusu Umoja wa Mataifa.