Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yemen kwenye hatari ya kukumbwa na njaa

Yemen kwenye hatari ya kukumbwa na njaa

Taifa la Yemen huenda likatumbukia kwenye hali mbaya ya kibinadamu wakati zaidi ya watu milioni 10 karibu nusu ya watu wote nchini humo wakiwa wanaandamwa na njaa. Viwango vya utapiamlo vinatajwa kuwa vya juu zaidi duniani wakati karibu nusu ya watoto wote walio chini ya miaka mitano nchini Yemen wakiwa na matatizo ya kukua na milioni moja wakiwa hawapati lishe ya kuwatosha. Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linaendelea na oparesheni zake na programu za chakula likilenga kusaidia watu milioni 5.5 ifikapo mishoni mwa mwaka huu. Tangu kuanza kwa mwaka huu hadi mwezi wa Julai watu milioni 3.4 walikuwa wamehudumiwa. Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP na anasema kuwa hali ya usalama inatatiza jitihada za kusaidia wanaotaabika nchini Yemen.

(SAUTI YA ELIZABETH BRYS)