Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatoa tahadhari ya ugonjwa mpya kote duniani

WHO yatoa tahadhari ya ugonjwa mpya kote duniani

Shirika la afya duniani WHO limetoa tahari ya ugonjwa usiofahamika kote duniani duniani ambao umesababisha kifo cha mtu mmoja huku mwingine akiwa hali mahututi hospitalini. Kulingana na WHO ugonjwa huo unasababishwa na virusi vinavyojulikana kama Coronavirus . WHO inasema kuwa ni machache mno yanayofahamika kuhusu ugonjwa huo yakiwemo maambukizi yake lakini hata hivyo unafahamika kuwa kwenye kundi la virusi vinavyojulikana kusababisha magonjwa kama mafua na homa hatari ya SARS. Inaripotiwa kuwa watu hao wawili walionyesha dalili na matatizo ya kupumu na kwenye njia za mkojo. Gregory Hartl kutoka WHO anasema kuwa virusi hivyo huenda vina mahusiano na taifa la Saudi Arabia kwa kuwa wote hao washasafiri kwenda taifa hilo nyakati tofauti.