Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yalaani mauwaji ya waandishi

UNESCO yalaani mauwaji ya waandishi

Umoja wa Mataifa umelaani vikali mauwaji ya waandishi wa habari waliouwawa katika matukio tofauti ikiwemo mmoja kuuliwa nchini Syria. Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na utetezi wa uhuru wa maoni UNESCO Bi Irina Bukova amesema kuwa kifo cha mwandishi wa habari Musab MohamedSaid Al-Oudaallah ambaye inadai aliuwawa mjini Damascas hapo August 22, ni cha kusikitisha na kukatisha tamaa juu ya mustakabala wa waandishi wa habari kwenye eneo hilo.

Amezitolea mwito mamlaka nchini Syria kujiepusha na matumizi ya nguvu dhidi ya waandishi wa habari na amewasisitizia namna wanavyopaswa kulinda uhuru wao wa kupasha habari. Kandoni mwa tukio hilo, Bi Bokova amelaani mauwaji ya waandishi wa habari wengine ambao wanaaripotiwa kuuwawa nchini Eretrea

Waandishi hao Dawit Habtemichael, Mattewos Habteab na Wedi Itay, walikamatwa tangu maka 2001 na waliendelea kusalia korokoroni hadi taarifa za vifo vyao zilipokuja hadharani