Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi Sierra Leone ndiyo kipimo cha kukomaa kisiasa:UM

Uchaguzi Sierra Leone ndiyo kipimo cha kukomaa kisiasa:UM

Uchaguzi mkuu nchini Sierra Leone uliopangwa kufanyika Novemba 17 mwaka huu ndiyo utatoa mwangaza wa kujua namna taifa hilo lilivyopevuka kisiasa.

Hayo ni kwa mujibu wa msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sierra Leone Jens Anders Toyberg-Frandzen wakati akizungumza kwenye baraza la usalama.

Bwana Toyberg-Frandzen amesema Sierra Leona inapiga hatua kusonga mbele na kunashuhudiwa mustakabala mwema baada ya kipindi kirefu cha vita.

Hata hivyo amedokeza mikwaruzano ya kisiasa iliyojitokeza katika kipindi cha miezi sita iliyopita na ameonyesha wasiwasi wa kujirudia kwa hali hiyo wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.