Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kunahitajika usawa katika kutoa nafasi za maendeleo:Ban

Kunahitajika usawa katika kutoa nafasi za maendeleo:Ban

Ushirikiano wa mataifa yanayopatikana Amerika ya Kusini na barani Afrika una uwezo wa kuleta usawa katika ukuaji kote ulimwenguni, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa ya ushirikiano wa mataifa ya kusini mwa dunia.

Bwana Ban amesema, hata wakati huu ambapo kuna matatizo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa, ushirikiano huo umeendelea kuchagiza maendeleo ya kibiashara na kifedha katika miaka ya hivi karibuni.

Amesema mataifa ya kusini yanajenga mienendo mipya ya ushirikiano wa maendeleo, ambayo inasisitiza faida kwa wote, pamoja na umoja na kupunguza gharama. Amesema hili linawasaidia watu kupata madawa, teknolojia na hata mikopo ya bei nafuu.