Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aelezea kusikitishwa kwake na hukumu kali dhidi wanaharakati wa kisiasa Bahrain

Ban aelezea kusikitishwa kwake na hukumu kali dhidi wanaharakati wa kisiasa Bahrain

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameelezea kusikitishwa kwake na hukumu kali, zikiwemo vifungo vya maisha, zilizohifadhiwa na mahakama ya rufaa ya Bahrain, dhidi ya wanaharakati 20 wa kisiasa. Ametoa wito kwa serikali ya Bahrain kuwaruhusu washtakiwa wote kutekeleza haki yao ya kuomba rufaa na kuhakikisha kuwa utaratibu unaofaa unafuatwa.

Bwana Ban amerejelea wito wake kwa serikali ya Bahrain kuhakikisha kuwa kanuni za kimataifa za haki za binadamu zinafuatwa, zikiwemo haki ya kuwa na hukumu yenye uazi na haki, uhuru wa kujieleza na kufanya maandamano ya amani.

Ametoa wito kwa serikali ya Bahrain kutekeleza kikamilifu mapendekezo ya tume huru ya uchunguzi ya Bahrain. Pia amesisitizia kauli yake kuwa, kunahitajika kuwepo mazungumzo ya kitaifa yanayowahusisha wote, na ambayo yatazingatia matakwa ya raia wote wa Bahrain, kama njia pekee ya kuendeleza amani, utulivu na haki katika nchi hiyo.