Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO, IFAD na WFP yahimiza hatua kukabili mfuko wa bei ya chakula duniani

FAO, IFAD na WFP yahimiza hatua kukabili mfuko wa bei ya chakula duniani

Hali iliyopo sasa katika soko la chakula duniani, ambayo inaonyesha ongezeko kubwa la bei ya mahindi, ngano na soyi, imeongeza hofu marudio ya tatizo la chakula duniani lililokuwepo mwaka wa 2007 na 2008. Lakini hatua ya haraka na ya pamoja kimataifa inaweza kufanya tatizo hilo lisiwepo tena, yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayohusika na chakula yakiwa ni FAO, IFAD na WFP.

Mashirika hayo yamesema ni muhimu kuchukuwa hatua ya dharura ili mfumko wa bei za chakula usije ukageuka kuwa janga litakalowafanya mamilioni ya watu kuumia katika miezi ijayo.

Yamesema matatizo mawili yanayohusiana ni lazima yatatuliwe, ambayo kwanza ni suala la sasa la mfumko wa bei ya chakula, ambalo linaweza kuathiri vibaya mno mataifa yanayotegemea kuagiza chakula kutoka nje na watu maskini zaidi, na pili, suala la muda mrefu la jinsi tunavyozalisha, kuuza na kutumia chakula katika kizazi hiki ambako idadi ya watu na mahitaji yanaongezeka, pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)