Mataifa lazima yakabili Chuki, Ghasia na Ubaguzi dhidi ya Roma:UM

2 Agosti 2012

Mataifa yote na hususani yenye jamii za Waroma lazima leo yaadhimishe kumbukumbu ya mauaji ya kikatili ya Waroma yaani Roma Holocaust, huku yakijikita katika kukabiliana na chuki, ghasia na ubaguzi dhidi ya Roma na kutafuta suluhu ya kutengwa kwa jamii hiyo.

Kauli hii imetolewa na wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na masuala ya walio wachache, ubaguzi, ubaguzi wa rangi, mauaji ya kulengwa na vitendo vya kutovumiliana. Mmoja wa wataalamu hao Rita Izsak ambaye mwenyewe ni Muhangary mwenye asili ya Roma anasema hakuchukuliwa hatua za kutosha kupinga ongezeko la chuki na ubaguzi dhidi ya Waroma barani Ulaya ambao unaziaibisha jamii. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud