Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yataka unyonyeshaji kwa kina mama urahisishwe

UNICEF yataka unyonyeshaji kwa kina mama urahisishwe

Katika maadhimisho ya 20 ya wiki ya unyonyeshaji duniani shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema sera imara za kitaifa kuunga mkono unyonyeshaji zinaweza kuzuia vifo vya takribani watoto milioni moja wa chini ya umri wa miaka mitano kila mwaka katika nchi zinazoendelea.

UNICEF inasema licha ya shahidi kwamba unyonyeshaji unazuia maradhi kama kuhara na nimonia ambayo huuwa mamilioni ya watoto kila mwaka bado kiwango cha unyonyeshaji duniani kimesalia bila mabadiliko makubwa katika nchi zinazoendelea ambapo kimeongezeka kidogo tuu kutoka asilimia 32 mwaka 1995 hadi asilimi 39 mwaka 2010.

Mkurugenzi mkuu wa UNICEF Anthony Lake anasema endapo unyonyeshaji ungekuwa unachagizwa vya kutosha na wanawake wangekuwa wanalindwa dhidi ya soko la maziwa mbadala basi dunia ingeshuhudia watoto wengi zaidi wakinurika na magonjwa na kungekuwa na kiwango kidogo cha utapia mlo na kudumaa.