Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uzalishaji wa madini ya chuma waongezeka kufuatia kuboreka kwa sekta ya chuma

Uzalishaji wa madini ya chuma waongezeka kufuatia kuboreka kwa sekta ya chuma

Ripoti kutoka kwa shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD inasema kuwa uzalishaji wa madini ya chuma uliongezeka mwaka 2011 kwa tani milioni 1.92 au asilimia 4.7 ikilinganishwa na mwaka 2010.

Ripoti hiyo inasema kuwa uzalishaji wa madini ya chuma uliongezeka kutokana na kuboreka ya sekta ya chuma ambapo uzalishaji wa madini hayo ulifikia tani 125. Kati ya wazilashaji wakuu, Australia iliongeza uzalishaji wake kwa asilimia 12.7 , Brazil kwa asilimia 5.1 na China kwa asilimia 2.1. Uzalishaji wa madini ya chuma nchini India ulipungua hadi tani 196 mwaka 2011 ikiwa ni kwa asilimia 7.5. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)