Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya Vikwazo Yajikita katika Tishio dhidi ya Al-Qaeida

Kamati ya Vikwazo Yajikita katika Tishio dhidi ya Al-Qaeida

Kufuatia mashambulizi ya kigaidi ya mwaka 1998 kwenye balozi za Marekani mjini Nairobi Kenya na Dar es salaam Tanzania , Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha vikwazo dhidi ya kundi la Al-Qaeida na Taliban.

Taliban walitimuliwa madarakani Kabul Afghanistan mwaka 2001, tangu wakati huo vikwazo vimeelekezwa kwa tawala wa Al-Qaeida popote ulipo amesema Richard Barrett mratibu wa kamati ya vikwazo dhidi ya Al-Qaeida.

(SAUTI YA RICHARD BARRETT)