Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majengo ya kihistoria kwenye pwani ya Panama yatajwa kuwa kwenye hatari ya kuangamia

Majengo ya kihistoria kwenye pwani ya Panama yatajwa kuwa kwenye hatari ya kuangamia

Kamati inayohusika na utamaduni duniani hii leo imeliorodhesha eneo moja nchini Panama kama moja ya maeneo yaliyo kwenye hatari kutokana na kutokuwepo utunzi unaohitajika , masusla ya mazingira na kuendelea kupanuka kwa miji. Eneo hilo lijulikanalo kama portobelo-San Lorenzo linatajwa kuwa mfano wa maeneo ya zamani ya kijeshi ya karne ya 17 na 18 yaliyojengwa kwenye pwani ya Panama kulinda biashara kwenye bahari ta Atlantic.

Kamati hiyo imesema kuwa eneo hilo lililoorodheshwa kuwa kati ya maeneo ya kitamaduni duniani mwaka 1980 linazidi kudidimia kwa haraka. Kamati kuhusu utamaduni hukutana mara moja kwa mwaka na ina jukumu la kutekeleza azimio la shirika la sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNICEF ya kutambua sehemu zinazostahili kuorodheshwa kama za kitamaduni duniani.