Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwindaji wa Vifaru Wapanda Kupindukia Afrika Kusini

Uwindaji wa Vifaru Wapanda Kupindukia Afrika Kusini

Takwimu mpya zilizotolewa na tume ya kimataifa kuhusu biashara katika viumbe waliomo kwenye hatari ya kutokomezwa, CITES, na Idara ya Mazingira ya Afrika Kusini, inaonyesha kwamba idadi ya vifaru wanawindwa imekithiri na kufikia kiwango kipya.

Idadi ya vifaru weusi mwituni inakadiriwa kuwa 5, 000 na ile ya vifaru weupe kukadiriwa kuwa 20, 000. Vifaru wa aina hizi mbili wanapatikana barani Afrika, na idadi yao ilipungua kwa kiasi kikubwa zamani. Mambo yalibadilika, na idadi hiyo ilipanda tena, hasa katika Afrika ya Kusini. Lakini kuongezeka upya kwa uwindaji katika miaka ya hivi karibuni kunaweka mafanikio hayo katika hatari kubwa.