Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uvumbuzi wa kibiashara unaweza kuboresha uchumi nchini Dominica:UNCTAD

Uvumbuzi wa kibiashara unaweza kuboresha uchumi nchini Dominica:UNCTAD

Uungwaji mkono ulio imara kwenye shughuli za uvumbuzi kwenye sekta za kibinafsi unaweza kuboresha uchumi nchini Dominica. Hii ni kulingana uchunguzi wa sera za sayansi, Teknolojia na uvumbuzi kwenye Jamhuri ya Dominica uliochapishwa hii leo na shirika la biasahara na maendeleo la Umoja wa Mataiafa UNCTAD.

Uchunguzi huo ulifanywa kwa ushirikiano na tume ya uchumi ya nchi za kusini mwa Amerika na Caribbean. Matokeo ya uchunguzi kama huo hutolewa na UNCTAD kwa ushirikiano na mashirika mengine baada ya ombi kutolewa na serikali za mataifa yanayoendelea.

Jamhuri ya Dominica inafanya jitihada za kusaidia biashara na taasisi zingine vikiwemo vyuo vikuu kiutumia sayansi na teknolojia kuboresha bidhaa zilizopo na kubuni zingine mpya.