Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watunuku mashirika 44 ya umma kwa huduma bora kwa jamii

UM watunuku mashirika 44 ya umma kwa huduma bora kwa jamii

Jumla ya mashirika ya umma 44 kutoka nchi 29 yanatarajiwa kutununukiwa wakati wa maadhimisho ya siku ya huduma kwa umma ya Umoja wa Mataifa ambayo itasherehekewa mnamo tarehe 23 mwezi huu.

Sherehe hizo ambazo pia zinaadhimisha mwaka wake wa kumi mwaka huu zitafanyika kwenye ukumbi wa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York. Siku hii ilibuniwa kupitia kwa azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kusherehekea huduma zinazotolewa kwa jamii.

Zaidi ya maombi 471 kutoka mataifa 80 wanachama wa Umoja wa Mataifa yalipokelewa mwaka 2012 huku mataiafa 16 zaidi yakishiriki ikilinganishwa na maombi yaliyotumwa mwaka 2011.