Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yalaani vikali mauwaji ya waandishi wa habari wawilli toka Uganda, Honduras

UNESCO yalaani vikali mauwaji ya waandishi wa habari wawilli toka Uganda, Honduras

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi na utamaduni UNESCO amelaani vikali matukio ya mauwaji ya waandishi wa habari wawili yaliyojiri katika nchi za Uganda na Honduras.

Mwandishi wa habari Alfredo Villatoro aliyekuwa akifanya kazi na kituo kimoja cha redio alikutwa amekufa nje kidogo ya mji wa Tegucigalpa,wakati Amon Thembo Wa’Mupaghasya, aliyekuwa mkurugenzi wa kituo cha tv Kasese nchini Uganda aliuwawa May 12.

Akijadilia matukio hayo Mkurugenzi wa UNESCO Irina Bokova amesema taarifa za kuuliwa kwa mwandishi wa habari Alfred Vikkatoro ambazo zimekuja wiki moja tu baada ya mwandishi mwingine kuuliwa zinaelezea hali halisi inayowaandama waandishi wa habari.

Amesema kuuliwa kwa waandishi hao wa habari kunakandamiza uhuru wa kujieleza na kuzidisha mbinyo na vitisho kwa wanahabari kote ulimwenguni.