Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za Asia-Pacific haziwezi kukua bila kushughulikia matatizo ya Mazingira:UM

Nchi za Asia-Pacific haziwezi kukua bila kushughulikia matatizo ya Mazingira:UM

Nchi za Asia na Pacific ziko njia panda na ni lazima sasa zitafute wiano baina ya kukuza maendeleo na ongezeko la uchaguzi wa hali ya hewa. Mafanikio au kushindwa kwao kathaari dunia nzima, inasema ripoti iliyotolewa Alhamisi na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP.

Ripoti inasema eneo la Asia Pacific ni lazima liendelee kukua kiuchumi ili kuwaondoa mamilioni ya watu kwenye umasikini, lakini ni lazima pia ishughulikie changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa ili kuweza kuishi. Suala la “kuka kwanza na kusafisha baadaye sio chago tena” inasema ripoti hiyo ambayo ni ya maendeleo ya binadamu kwa kanda ya Asia-Pacific kwa mwaka 2012, iitwayo “dunia moja ya wote, kukuza maendeleo ya binadamuu katika mabadiliko ya hali ya hewa”. Amr Nour ni mkurugenzi wa ofisi ya kanda ya New York inayohusika na utafiti wa uchumi na masuala ya kijamii katika eneo la Asia na Pacific.

(SAUTI YA AMR NOUR)

Ripoti hii kwa mujibu wa UNDP ina lengo la kuchagiza majadiliano ya mabadiliko ya hali ya hewa kwa kuleta pamoja masuala yote yanayowatia watu hofu katika wakati huu wa maandalizi ya mkutano wa Rio+20.