Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hofu kufuatia kuuawa kwa mwandishi habari nchini Mexico:OHCHR

Hofu kufuatia kuuawa kwa mwandishi habari nchini Mexico:OHCHR

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea wasi wasi uliopo kufuatia kuuwa kwa mwandishi mwingine wa habari nchini Mexico. Regina Martinez alipigwa risasi na kuuawa wiki iliyopita. Mashirika ya haki za binadamu yanasema kuwa mauaji hayo yanavuruga uhuru wa kujieleza nchini Mexico baada ya zaidi ya waandishi 70 kuuwa nchini humo tangu mwaka 2000.

OHCHR imetaka kufanyika kwa uchunguzi ulio huru kuhusu mauaji haya na kuitaka serikali ya Mexico kuchukua hatua za kuwahakikishia usalama waandishi wa habari. Hata hivyo kamishna mkuu wa haki za binadamu amekaribisha kupitishwa kwa sheria mpya zinazolinda watetesi wa haki za binadamu na waandishi wa habari anavyoeleza Rupert Colville wa ofisi ya haki za binadamu.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)