Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atoa ripoti yake juu ya maambukizi ya virusi vya HIV

Ban atoa ripoti yake juu ya maambukizi ya virusi vya HIV

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa ripoti yake ya kwanza inayoangazia hali ya maambukizi ya virusi vya HIV ikiwa imepita mwaka mmoja tangu kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa ngazi za juu waliomulika ugonjwa wa Ukimwi.

Akitoa ripoti hiyo mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Ban amedokeza haja ya kuwajibika kwa haraka ili kuyafukia malengo halisia ya kukabiliana na tatizo la ugonjwa huo.

Kwenye ripoti hiyo Ban amependekeza mbinu na hatua ambazo amesema kuwa lazima zizingatie pia uweledi, mipango makini ambayo pia lazima ifungamane na haki za binadamu.

Hata hivyo amehimiza jumuiya ya kimataifa kuanza kutekeleza kwa vitendo ahadi iliyoweka hapo kabla kwa shabaha ya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo.