Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kuanzisha oparesheni za usambazaji chakula nchini Senegal

WFP kuanzisha oparesheni za usambazaji chakula nchini Senegal

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linatarajiwa kuzindua operesheni ya usamabazaji wa chakula kwenye sehemu za vijiji kwenye eneo la Oukout nchini Senegal. Akihutubia mkutano wa waandishi habari mjini Geneva Elizabeth Byrs kutoka shirika hilo anasema kuwa eneo hilo ni moja ya sehemu zilizoathirika zaidi na ukame nchini Senegal ambapo karibu nusu ya watu wanakabiliwa na njaa.

WFP inatarajiwa kutoa misaada kwa watu 739,000 kwenye sehemu za vijijini na watu wengine 67,000 sehemu za mijini nchini Senegal. WFP pia inatarajiwa kutoa lishe kwa zaidi ya watoto 100,000 waliokabiliwa na utapiamlo pamoja na akina mama. Hadi sasa inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni mmoja hawana usalama wa chakula nchini Senegal.